Friday, May 20, 2011

HIVYO WAKULIMA HAWA WANAPATA FAIDA NA MAZAO YAO?

 Blogu hii leo imepita katika soko la mazao ya chakula SODECO Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma na kukuta shehena ya magunia ya mahindi ya msimu huu mengine yamelazimishwa kukauka ili wayauze kwa walanguzi kwa bei ya hasara.Lakini nilikutana na mkulima mmoja alisema mahindi hayo ya mwaka huu yanaizwa kwa sababu ya shida.
Akaendelea kusema kuwa wanalazimika kuuza kabla ya musimu wa kuyauza kwenye ghala la chakula la taifa kwa kuwa watoto wanahitaji ada,sare na matibabu.Mkoa wa Ruvuma mwaka huu utakuwa na mavuno makubwa ya mahindi ikilinganishwa na musimu uliyo pita.

No comments:

Post a Comment