Wednesday, May 11, 2011

TANROADS WAOMBWA KUWEKA LAMI BARABARA YA KWENDA DARAJA LA MKENDA


Mbunge akumbusha TANROAD kuweka lami Barabara ya kwenda daraja la Mkenda la Umoja  Tanzania na Msumbiji

MBUNGE wa Jimbo la Peramiho Mhe.Jenista Mhagama amewakumbusha TANROAD kuwa Rais Jakaya  Kikwete alisema  barabara iyendayo kwenye daraja la Mkenda litawekwa lami ili iweze kupitika katika msimu wote wa mwaka.

Alisema hayo kwenye kikao cha barabara TANROAD kilicho fanyika katika ukumbi wa Songea Club leo,alisema daraja hilo ni himu sana kibiashara kati ya Tanzania na Msumbiji,ambapo sasa magari yanatoka Msumbiji kuja Tanzania na Tanzania kwenda Msumbiji.

Aliwaomba TANROADS kufuatilia ahadi aliyo sema Rais Jakaya Kikwete wakati akizindua ujenzi wa daraja hilo mwaka uliyopita ya kuwekwa lami barabara.

No comments:

Post a Comment