Friday, June 28, 2013

WACHAPAJI WAKUMBUSHWA WAJIBU WA NA UTARATIBU WA UTENDAJI KAZI KATIKA UTUMISHI WA UMMA


Bwana Stephen Pancras akitoa mada kwa wakuu wa vituo vya kanda juu ya wajibu wa mfanya kazi kiongozi,mfanyakazi na kujua wajibu wao na haki kwa wafanya kazi zilizo fafanuliwa katika sheria kadhaa.
Alizitaja sheria hizo kuwa ni pamoja na Sheria ya kazi na mahusiano,Sheria ya majadiliano,Sheria za Taasisi  za kazi,Sheria za Utumishi wa Umma,Kanuni za kudumu katika Utumishi wa Umma na Miongozo mingine.





 Washirki wakiwa katika mada ya Utumishi wa Umma
 Sekretarieti ikifanya samari ya mada hiyo ambao pia ni wakuu wa vituo vya Kanda,Kulia ni Bi.Josephine Sanga Mkuu wa kituoa Moshi,Wakatikati mwenye Suti nyeusi Bw.Juma Nyumayo Msaidizi wa Mkuu wa kituo Kanda ya Kusini Songea na watatu ni Bw.Mahimbo Mkuu wa kituo Tabora.
 Mkuu wa Kituo Press A na Mkuu wa vytuo 7 vya kanda vya elimu nchini Bw.Max Masesa akimkaribisha mtoa mada hayupo katika picha katika Warsha hiyo katika ukumbi wa ADEM Bagamoyo hivi karibuni
 Washiriki
 Washiriki
Bwana Stephen Pancras akitoa mada kwa wakuu wa vituo vya kanda juu ya wajibu wa mfanya kazi kiongozi,mfanyakazi na kujua wajibu wao na haki kwa wafanya kazi zilizo fafanuliwa katika sheria kadhaa.
Alizitaja sheria hizo kuwa ni pamoja na Sheria ya kazi na mahusiano,Sheria ya majadiliano,Sheria za Taasisi  za kazi,Sheria za Utumishi wa Umma,Kanuni za kudumu katika Utumishi wa Umma na Miongozo mingine.

USIRI KATIKA UCHAPAJI WA NYARAKA ZA SERIKALI NA WATU BINAFSI NI WA LAZIMA - MNJAGILA

Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi Bw.Salum Mnjagila akiongea na Wakuu wa vituo vya Kanda pamoja na watendaji wao katika ukumbi wa ADEM Bagamoyo hivi karibuni
Washiriki wa Warsha hiyo
Washiriki  wa Warsha hiyo
Mkuu wa Chuo na Mtendaji wa Chuo ADEM Dkt.Siston Masanja akizungumza na wana Warsha katika ukumbi wa chuo hicho.
Washiriki wa Warsha hiyo
Wakiimba wimbo wa mshikamano kazini

Wakiimba wimbo wa wafanya kazi
Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi, Bwana Salum Mnjagila amewataka wakuu wa vituo vya uchapaji vya Kanda  vya Elimu Nchini na watendaji wao kuwa makini katika usiri wa kazi za watu zinazopelekwa kwenye vituo hivyo.
Bw.Mnjagila alisema hayo wakati wa akifungua Warsha ya siku moja kwa Viongozi na watendaji kutoka makao makuu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na wakuu wa vituo vya Kanda na watendaji wao katika Ukumbi wa ADEM Bagamoyo hivi karibuni.
Alisema Warsha hiyo ilikuwa ya muhimu sana kwakuwa imewakutanisha watumishi wote pamoja na viongozi wao mahali pamoja kwa lengo la kukumbushwa wajibu wao katika masuala ya machapisho mbalimbali ambayo yana hitahi usiri mkubwa.
Machapisho ambayo aliyataja Mkurugenzi huyo ni pamoja na TSM 9, mitihani ya Mock za mkoa, Mock za sekondari, Mitihani ya darasa la nne ya Taifa , Mithani ya Kidato cha pili, pamoja na nyareka mbalimbali za watu binafsi.
Aidha Mkurugenzi aliomba ushirikiano kati ya ADEM na Elimu ya Watu Wazima udumishwe kwakuwa ni vitu vinavyo tegemeana, kwa kuanzisha kozi wakishirikiana na VETA ya uchapaji na masuala yote yanayohusu Printing Press.
Awali Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha ADEM Bagamoyo Dkt.Siston Masanja alielezea kwa ufupi Taasisi yake kuwa iko chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi,na inatoa kozi za muda mrefu na muda mfupi katika ngazi mbalimbali za kielimu.
Alisema kuwa ushirikiano uliopo katika ya ADEM ni wa kudumu ,ambapo aliwashukuru Mkurugenzi pamoja na Naibu Mkurugenzi  Kisomo Mwanza kwa kutoa fursa ya kutoa kozi hizo kwa wanafunzi wanaosoma kisomo.
Naye Mkuu wa Kituo cha Uchapaji Press A na Mkuu wa vituo vya uchapaji vya Kanda Bwana Maxmilian Masesa.Alimshukuru Mkurugenzi na Naibu Mkurugenzi Kisomo Mwanza kwa kukubali kwao,kufanya Warsha ya kihistoria ya kuweza kujumuisha viongozi wote pamoja na watendaji wao mahali pamoja kwa lengo la kuleta maendeleo na ushirikiano  katika vituo hivyo.
Aidha alimshukuru Mkuu wa Chuo cha ADEM pamoja na Uongozi mzima wa chuo hicho kwa kukubali kwao kuruhusu warsha hiyo kufanyika pale kwa amani na utulivu mkubwa uliyojitokeza.

Thursday, June 13, 2013

SERIKALI YATARAJIA MAKUSANYO YA TRIONI 18.2 MWAKA WA FEDHA WA 2013/2014

SERIKALI inatarajia kukusanya shilingi Trioni 18.2 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya mapato katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 iliyosomwa lieo Bungeni mjini Dodoma.