Wednesday, August 31, 2011

SIKUWEKO KATIKA MTANDAO KWA MUDA NILIKUWA SAFARINI MBEYA ,TULIPUMZIKA MAKAMBAKO

Tulisimama kupata chai na wengine walikwenda kuchimba dawa,ingawa si jambo la kawaida kuchimba dawa mjini.bali ni lugha laini ya kwenda kujisaidia.MakambakoMkoa wa Njombe tukielekea Mbeya na Bus la Supar Feo .Hivyo kuanzia kesho nitakuwepo hai katika mtandao ni kija na mwana mazingira mkoani Ruvuma.

VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUKEMEA MATENDO MAOVU



RAIS Jakaya Kikwete amewataka viongozi wa madhehebu ya dini nchini kishirikana na serikali katika kukemea maovu yakiwemo ya biashara ya madawa ya kulevya ambayo yana haribu vijina ,pia wanafunzi wa shule za msingu,sekondari amabo ndiyo nguvu kazi ya Taifa.
Rais Kikwete alisema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Baraza la Eid iliyofanyika  kitaifa katika Msikiti wa Mkoa wa Dodoma leo akiwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za Eid,l alisisitiza kuwa ni wajibu wake kukemea,kuonya na kutahadharisha hatari itakayo kuja mbele yake.
Alisema kuwa tahadhari hiyo aliitoa siku ya kumweka wakfu askofu Jonh Ndimbo wa jimbo la Mbinga kuwa baadhi ya viongozi wa dini wanajihusisha na madawa ya kulevywa na wengine walishikwa,wakiwemo watoto wa viongozi wa madhehebu ya dini.’Ilikuwa ni wajibu wangu kukemea na tahadharisha wimbi la bishara ya madawa hayo kuingia katika madhehebu ya dini’ alisisitiza Rais.
‘Viongozi wa madhehebu ya dini zote tushirikiane katika mapambano haya ya kukemea maovu yanayo sababishwa na biashara hii.’ Alisema Rais.Hili ni tatizo kubwa tunaomba tushirikiane alisisitiza tena Rais.
Aidha katika Baraza hilo la Eid Rais alisema kuwa Serikali ina Mahakama yake hivyo haiwezi kuunda mahakama nyingine,alipokuwa akiwaeleza Waislamu kuwa jambo la Mahakama ya kadhi  bado linaendelea,anashughulikia Waziri mkuu ,wala hakuna mkono wa mtu.
Alisema suala hilo litajadiliwa Bungeni,na Bungeni hakuna siri,kila mmoja atakuwa na nafasi yake ya kuchangia suala hilo,wala siyo shinikizo la Baraza la Maskofu ila wao walicho kisema nikuwa suala hilo liachiwe kwa waislamu wenyewe na siyo serikali kuingilia musuala ya kidini.
Alisema lengo la mahakama hiyo ni kwa ajili ya Talaka,Mirathi na wafu,si zaidi ya hayo masuala yote yakijinai,madai,wizi yaachiwe kwenye mahakama ya serikali na siyo mahama ya kadhi.

Monday, August 22, 2011

WANAOWANIA KITI CHA UMEYA KATIKA MANISPAA YA SONGEA WAMEJITOKEZA

Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea,baadhi yao wamejitokeza kuwania nafasi ya Umeya iliyowachwa wazi na Marehemu Ally Manya aliyefariki hivi karibuni.Kati yao kuna wanawake wawili wamejitosa katika kinyang'anyiro hicho.

KATIKA PITA PITA YANGU LEO NIKAKUTANA NA MKURUGENZI WA MAZINGIRA AKIHOJIWA NA MWANDISHI WA HABARI ( PST )

Mkurugenzi wa Mazingira Bwana Metodi Ngerangera mwenye koti nyeusi na mwandishi wa habari wa magazeti ya Nipashe Bwana Gedion Mwakanosywa mwenye miwani,wakiwa nje ya hotel ya Ok.
Bwana Ngerengera amehamasisha shule 18 kupanda miti,mbali mbali katika kuhifadhi mazingira ya shule hizo,Anasema wakati mwingine anatumia fedha zake mwenyewe katika kuboresha mazingira ya shule,zaidi nitakuletea shughuli nyingine anazozifanya tofauti na utunzaji wa mazingira.

JUMATATU HII NILIKWENDA KUTEMBELEA HOTEL YA OK HAULE KATIKA MANISPAA YA SONGEA

 Bwana Ok Haule ndiye mkurugenzi wa Hotel hiyo  maarufu sana,katika Manispaa ya Songea ni kwa sababu ipo karibu na soko kuu la Songea,unapata mazali na chakula .Amesimama kwenye mlango aliyoufanyia ukarabati  ili hotel  ilingane na hadhi na mahitaji ya soko.
Huyu ni fundi wake wa kuandaa na kuiweka sawa miundo mbinu ya hitel hiyo iliyoko karibu na kanisa la KKT mjini hapa.

Saturday, August 20, 2011

HII NDIYO STENDI YA MANISPAA YA SONGEA LEO NA SAFARI ZA VIJIJINI NA HOSPITALI YA PERAMIHO MKOANI RUVUMA

 Ni mabasi madogo yaendayo Makamboko ya Super Feo ambayo huondoka hapa mchana nakuingia Makambako jioni.
Hayo ni mabasi madogo ambayo yanafanya safari za kwenda Peramiho na kurudi mjini Songea kila wakati,Peramiho kwenye hospitali ya Wamisionari wagonjwa huenda kupata matibabu na wengine wanakwenda kuona ndugu zao  waliyolazwa katika hospitali hiyo.

Wachanga shilingi 200,000 kupeleka kwa Binti Ndembo kumfichua mwalimu Athuman aliyepotea



WANANCHI wa Kata ya Msamala Kijiji  cha Msisima wamechangisha jumla ya shilingi 200,000 ili kuzipeleka kwa mganga wa jadi al maarufu kwa jina la Binti Ndembo aliyoko kilometa chache kutoka Mmanispaa ya Songea,ili aweze kumfichua mwalimu Athuman Athumani waliye potea mjini Songea.

Akizungumza na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi jina la shule halijulikani Bwana  Hamisi Hongo alisema mwalimu huyo alipotelea Mjini Songea mwezi Aprili mwaka huu akiwa na walimu wenzake kwenda kupokea mishahara yao na kufikia Guest House tofauti.

Walimu hao waliyefuatana naye mwalimu huyo walisema baada ya siku ya 4 walifika kwenye nyumba hiyo wa wegeni ambayo hawakuitaaja jina lake,waliambiwa mwalimu huyo hakuwepo katika chumba alicho chukua isipokuwa begi lake.

Mke wa mwalimu huyo Bibi Asha Jafari alipokwenda kwa Binti Ndembo aliambiwa kuwa mmewe yupo hai,hivyo kiasi cha fedha hizo kitalipwa kwa mganga huyo ili aende nyumbani kwa mwalimu huyo ili awatajie alikokuwa na jinsi ya kumrudisha.

Aidha kaka wa mwalimu huyo Bwana Saidi Athumani naye alipotea mwaka 2008 katika mazingira ya utata hadi habari hizi zinaletwa kwenye Blog hii hajulikani aliko.
( Source Fashen Milasi /Msisima Lusewa Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma )

Friday, August 19, 2011

BREAKING NEWS !11!!! RAIS KIKWETE KUTOA TUZO KWA WATAALAMU WA MADAWA YA MARELIA

 Rais Kikwete alisema kuwa matumizi ya dawa ya mseto na  vyandarua yamesaidia kupunguza vifo vinavyo tokana na marelia.Alisema hayo alipokuwa akiongea na wataalamu wa afya hivi karibuni Jijini Dar es salaam.
wageni waliyokuwa kwenye sherehe hiyo.
 Picha ya pamoja ya Rais Jakaya Kikwete na wataalamu hao waliyo shika zawadi zao ( Tunzo )
 Kiongozi wa wataalamu hao akiongea baada ya Rais kuzungumza
 Rais anamkabidhi tunzo mmoja wa wataalam hao
Baadhi yao wakibadilishana mawazo wakati  wa sherehe hiyo ambayo TBC Taifa ikifanya kazi ya kurusha shughuli nzima za sherehe hiyo muhimu kwa Taifa.

BREAKING NEWS ! ! KASHESHE LA UKOSEFU WA UMEME JIJINI MWANZA SIKU NNE LAZUSHA BALAA KWA WATUMIAJI

 Jiji la Mwanza ama Rock City limekosa umeme kwa siku nne mfulululizo na lisabibishia Jiji hilo hasara kubwa kwa watumiaji wa umeme katika shughuli za uzalishaji mali.Mtumiaji huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana nasema kuwa kumekuwa na shida ya usagaji wa nafaka,hivyo watu wanahangaika kupata unga.
 Bibi huyo naye anasema maji yamekuwa shida baada ya mashine za kusukuma maji kushindwa kufanya kazi kwa ukosefu wa umeme,hivyo akina mama imewalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni kuisaka ndoo moja ya maji.
Ukizingatia jiji hilo ni la viwanda imekuwa ni hasara kubwa iliyopatikana kwa siku hizo nne,Huduma za matibabu ya upasuaji nayo imekuwa shinda.Ni kweli Sipika wa Bunge alikuwa sahihi kuitaka serikali itoe ufafanuzi wa sakata hilo la umeme Mwanza na Arusha,

Thursday, August 18, 2011

MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI MHE.FREEMAN MBOWE AMSIKILIZA KWA MAKINI WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII

 Mheshimiwa Freeman Mbowe akimsikiliza kwa makini Waziri wa maliasili na Utalii Mhe.Ezekiel Maige wakati akihitimisha Bajeti yake jioni hii leo Bungeni mjini Dodoma.
Mhe.Maige akisisitiza kuwa yote yaliyochangiwa na wabunge katika kuboresha na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika wizara yake atayafanyia kazi mara baada ya bajeti yake kupita.

MKURUGENZI WA MALIASILI NA UTALII ASIMAMISHWA KAZI NA KULIPWA MSHAHARA NA WENZAKE WAWILI

 Waziri wa maliasili na utalii Mhe.Ezekiel Maige aliliambia Bunge leo kuwa Mkurugenzi wa Maliasili na Utalii Bw.Obed Mbangwa na wasaidizi wake wawili wamesimamishwa kazi leo tarehe 18/8/2011 kutokana na maombi ya baadhi ya wabunge kwa serikali kumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo wakati uchunguzi unaendele kufanyika wa utoroshwaji wa wanyama,utoaji wa vibali kiholela.
 Mhe.Maige asisitiza kuwa migogoro ya mipaka katika hifadhi na utaratibu wa kutolewa kwa vitalu vya uwindaji itashughulikiwa.
Wabunge wamekuwa wakitaka kuwa huduma zinazotolewa na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro iangaliwe upya.

SERIKALI IMEPIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI WA WANYAMA HAI KWENDWA NJE YA NCHI

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda leo ameliambia Bunge Mjini Dodoma kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Mhe. Pinda kuwa Srikali imesitisha usafirishaji wa wanyama hai kwenda nje ya nchi.Serikali imegundua kuwa taifa linapata hasara kubwa kwa wajanja wachache wenye tabia ya kutorosha wanyama,bila ridhaa ya serikali.
Hilo ndilo Bunge,wakati Waziri,au mtoa hoja akiwa anatoa hoja yake,utakuta wabunge nao wnateta jambo wakati bunge linaendelea,hivi hawa wabunge ambao Waziri anawakilisha bajeti yake au Mbunge anatoa hoja yake wao wanazungumza vivyo Sipika wao ni yupi?,hivyo kinacho wakilishwa wanakielewa kweli? ingekuwa Sipika wa Bunge angekuwa anawauliza wabunge hao nini kilicho wakilishwa wangeweza kujibu kweli?

MATUKIO !!! MIZANI ISIRUHUSU MAGARI YALIYOBEBA MIZIGO MIZITO - KIWETE

 Rais Kikwete alisema kuwa mizani isiawaonee aibu wenye kuzidisha uzito kwenye magari yao makubwa,maana magari yenye mizigo mikubwa uhatarisha usalama wa barabara.Aidha kwenye mizani kuna vitendo vinavyo ashiria rushwa ,mwenye dereva humtuma tan boy kwennda kusafifha njia kwa kutoa kitu kidogo,kitu kidogo,ni aibu kwa taifa letu,Alisema nchi nyingi zinapitisha mzigo yao kwenye barabara zeto.alisema hayo kwenye uzinduzi wa barabara lami kutoka Usagara mwanza kuelekea GEITA.
 Rais Kikwete alikuwa akizindua barabara hiyo hivi karibuni Jijini Mwanza
Barabara kiwango cha lami toka Usagara hadi Geita.

Wednesday, August 17, 2011

kawaida ya binadamu pale mwenzake anapofanya vizuri kumsifia ni muhimu,Hivi TANROAD wa Mkoa wa Iringa nitofauti na wengine?


 Hongereni Wizara ya Miundombinu hivyo Mikoa yote ingeweza kufikia kiwango cha barabara kama hiyo ya kuingia mjini Iringa situngejisifia sana!.Hivyo TANROAD wa Iringa ni tofauti na TANROAD wa Mikoa mingine?
 Hiyo ndiyo kazi za watengeneza barabara kwa viwango hata usiyekwenda shule utagundua kazi nzuri iliyofanywa.
Watu wanapofanya kazi nzuri tuwasifie na wengine tuige ,maana wa - tanzania tunatabia ya kusifia sifia vya wenzetu lakini vyetu hatuvioni kuwa ni vyema.

TWIGA SI PANYA AMABAYE UNAWEZA UKAMFICHA NA KUMSAFIRISHA, INASHANGAZA TWIGA WETU WANASAFIRISHWA NA NDEGE UWANJA WA KIA ,KWENDA NJE HUKU TUNAONA.

Mchungaji Peter Simon Msigwa wa Iringa Mjini ( CHADEMA ) anashangazwa na aina ya usafirishaji wa wanyama wakubwa kama twiga kutolewa katika hifadhi hadi uwanja wa ndege wa Kia  kama wanayama wadogo kama panya asiyeweza kuonekana na kusafirishwa nje ya nchi.Hivyo ndiyo uwekezaji huo?,huo sio wizi wa wanyama wetu ?.

Aidha Mhe.Msigwa alisema kuwa lazima serikali ibadilishe mfumo uliyo kuwepo katika wizara ya maliasili na utalii uliyokuwepo.Maana waliyopewa dhamana wamepoteza uzalendo,watu waache kujinufaisha wenyewe badala ya kulinufaisha taifa.( Source Jambo Tanzania TBC )

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro haiwatendei hakiwafugaji

Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Ole Telele aliimbia Jambo kipindi kinachorushwa na TBC  leo kuwa,Mbuga ya Ngorongoro ndiyo mbuga pekee duniani ambayo kunahifadhi na binadamu ( wafugaji ) naoishi katika Hifadhi hiyo.

Mhe.Telele alisema Serikali kupitia Mamlaka ya hifadhi hiyo haiwatendei haki wafugaji wanaishi katika mamlaka hiyo kutokana na kupewa fedha kidogo ukilinganisha na mabilioni ya fedha yanayo kusanywa.Kwa mtindo huo wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo hawanufaiki na mifadhi husika.

Tuesday, August 16, 2011

Wasanii wa Nyimbo za Injili wanainjilisha ,pia wananufaika kwa kazi yao ya sanaa.

Kwaya ya Remera SDA Churh - Kigali  Rwanda  na nyimbo zao za Kwetu Pazuri ambayo sasa inatamba sana wameimba kwa kutulia sana.

BREAKING NEWS DKT.MOHAMED GHARIB BILALI ZINDUA NYUMBA ZA ASKARI POLISI JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilali jana amezindua nyumba za askari polisi zilizoko Jijini Dar es salaam.
Ni kati ya nyumba za askari polisi zilizozinduliwa jana na Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilali Jana.

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LINA JENGA NYUMBA KWA KILA MWANANCHI ANAYE HITAJI NYUMBA

Mkurugenzi mkuu wa shirika la nyuma la Taifa Nehemiah Mchechu alisema shirika lake linajenga nyumba ambazo kila mtanzania mwenye mahitaji ya nyumba ataweza kupanga au kununua,bila ya kujali kipato cha mtu ili aweze kutimiza masharti ya ununuzi ama upangaji wa nyumba hizo.

Alisema hayo leo kwenye kipindi cha kutoka Dodoma kinacho rushwa na TBC asubuhi.

SHIRIKA LA NYUMBA LINAWEZA KUTENGEZA AJIRA KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM

Mheshimiwa John  Momose Cheyo aliema kuwa shirika la nyumba la Taifa linaweza kutengeneza ajira kwa vijana wa Jijini Dar es salaam iwapo itapata ardhi kubwa nje ya jiji na kuanza kujenga nyumba zinazo weza kununuliwa kwa kila mtanzania kutokana na vipato vyao.

Alisema hiyo itawezekana iwapo serikali itaondoa VAT kwenye vifaa vya ujenzi,alisema kuwa si wakati wa watanzania kugawana umasikini,ila ni wakati wa kugawana utajiri kama shirika litajenga nyumba kulingana na soko.Alisema hayo kwenye kupindi cha leo toka Dodoma kinacho rushwa na TBC.

ULIMWENGU WA KISWAHILI,KAMA UNAMSAMIATI UNAOKUTATANISHA UPELEKE SIMU NAMBA 0784815651 UTAPATA JIBU

 Ulimwengu wa kiswahili ni kipindi kinachorushwa TBC Kuchambua na kusanifu lugha ya kiwsahili,Mwenyekiti wake ni Mzee Seleman Hega wajumbe ni pamoja na Profesa Abdallah Jumbe Safari,Profesa Masamba na Mwalimu Mohamed Mwinyi
 Mwenyekiti Seleman Hega
Profesa Safari mwenye kofia na Profesa Masamba mwenye koti.kama una neno la kiswahili lina kuletea utata,wapigie simu namba 0784 - 815651 watalichambua kwa makini na utaalamu wa lugha ulivyo.Kiswahili si lugha nyepesi kama tunavyo fikiri ndiyo maana wapo hao maprofesa wa lugha hiyo.

MANISPAA YA SONGEA LEO JUMANNE ,WATU NA HEKAHEKA ZA MAISHA

 Hiyo ni Manispaa ya Songea leo
 Daladala zikisubili wasafiri
Haya ni maeneo ya soko kuu mjini hapa

MASHINE YA UMEME ILIYO AHIDIWA NA KIKWETE KWA WAKAZI WA SONGEA KUWASILI DAR ES SALAAM MUDA MFUPI KUANZIA SASA

 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ruvuma Injinia Monica Kebera akizungumza na waandishi wa habari wa Blog ya TUJIFUNZE KUSINI ofisni kwake leo.kuhusu Rais Kikwete alivyo tekeleza ahadi yake kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma ya kutatua tatizo la umeme katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kuleta mashine mpya ya kuzalisha umeme.



Injinia Kebera akipata uhakika wa lini mashine hiyo itawasili Nchini katika bandari ya Dar es salaam kutoka Netherlands.kwa njia ya simu. ofisini kwake leo katika Manispaa ya Songea.




AHADI ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kiwete ya kupeleka mashine ya kufua umeme Manispaa ya Songea katika kituo cha kuzalisha umeme  ( Power Station )Kiblang’oma Lizaboni Manispaa ya Songea ameitekelea ya kuileta mashine hiyo ambapo muda wowote kuanzia sasa itawasili bandari ya Dar es salaam.
 Akizungumza na Blog ya TUJIFUNZE KUSINI ofisini kwake leo meneja wa TENESCO Mkoani Ruvuma Injiania Monica Kebera alisema mashine hiyo ni mpya yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa KW 1,900 ambayo itawasili bandari ya Dar es salaam tarehe 26 mwezi huu kutokea Neither land.

Injinia Kebera alisema mahitaji ya umeme kwa watumiaji wa Manispaa ya Songea ni KW 4,500,ambapo mashine hiyo ikifungwa tatizo la umeme litapungua kwa kiasi ingawa mgao utaendelea kuwepo kutokana na tatizo la taifa la upatikanaji wa mafuta na mashine kufanyiwa matengenezo.

Alisema mataizo ya mgao wa umeme ni wanchi nzima ila kwakipindi kilicho jitokeza cha kukosa umeme kabisa mjini hapa ilikuwa ni kwa sababu ya ubovu wa mshine zake Kibulang’oma na  upatikanaji wa mafuta kwa wakati.

Aidha Ijinjia Monica amemshukuru Rais kwa ahadi yake aliyoitoa kwa wakazi wa mkoa wa Ruvuma ya kuleta mashine mpya ya kuzalisha umeme ameitekeleza kwa wakatu mwafaka ,hata wakati tukisubiri umeme wa grid ya Taifa lakini watumiaji wa umeme watakuwa wana matumaini makubwa ya kupata umeme wa uhakika.

Monday, August 15, 2011

BREAKING NEWS LEO BUNGENI KULIPENDEZA KWELI PALE WALIPO HOJI HATI MILIKI YA KIWANJA IWEJE ICHUKUE MIAKA NANE? NA YA CHAP CHAP SIKU MOJA AU MBILI? NA UGONJWA HUO UPO SDA DODOMA

 Mheshimiwa Hassan Zungu alisema kuwaondoa wakazi wa Jangwani ni kuwanyanyasa,kuwa pale hawakupenda ila hali yao ya kipato,alisema wako pale si kutaka utajiri bali ni kuwasomesha watoto wao.
 Waheshimiwa wabunge hao walikuwa wakichangia bajeti ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi.Ukweli wizara hiyo kuna ujanja ujanja unafanyika hasa katika upataji wa ofa na hati utazungushwa sijui ili ukate tamaa.
o
 Ukweli inawaathiri sana watu wasio na kipato kwa ajiri ya kununulia haki yako,masikini pesa yaziada ya kutoa ili upate ofa au hati itatoka wapi.Cha ajabu wanaohusika wanasikia na kilio cha wabunge ambao ndiyo wawakilishi wa wananchi wanavyotetea.
 kila mmoja alichangia kutokana na hali anavyoiona na mapungufu ya wizara hiyo
 Mbunge wa Mtwara Mikindani anasema ili manispaa hiyo iwe ni lazima kata za Ziwani na Namayanga za Mtwara vijijini zipelekwe Mjini anauliza kigugumizi kiko wapo kwa serikali,alisema Mikindani ni Mji wa Kihistoria
Mbunge wa Kigamboni Dar es salaam anauliza hatima ya wakazi wa kigamboni iko wapi,wapo wananchi wenye uwezo wanaweza kuwekeza,na wale wenye uwezo mdogo wawe wabia na wawekezaji watakao wekeza kigamboni.