Tuesday, May 10, 2011

MKOA WA RUVUMA NA MIKOA MICHACHE TANZANIA NDIYO ZIMEPATA MVUA MWAKA HUU

Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe.Jenista Mhagama amesema mharibifu wa mazingira si rafiki wa mazingira kwani watakaribisha jangwa katika mkoa huo.alisema mwaka huu mkoa wa Ruvuma na mikoa michache sana nchini ndiyo iliyo pata mvua za uhakika.mingine mvua hazikuwa za uhakika hivyo hali ya chakula ni mbaya katika mikoa hiyo.


Aidha amesema kuwa katika ziara yake amekuta wakulima wa tumbaku ambao hulima zao hilo kama zao la biashara,ila elimu ya kutunza mazingira ielekezwe kwa wakulima wanao kata miti kwa ajili ya tumbaku hiyo hasa katika Wilaya ya Namtumbo.


Alisema ili kuepuka walanguzi kuwaibia wakulima mazao hasa mahindi ni vizuri kuanzishwe maghala ya kununulia mahindi ya wakulima kule waliko.

Pia aliomba maghala ya Mpitmbi,Litisha na Lusonga NAFRA Ruvuma kwenda kununua mahindi katika maghala hayo.


Vilevile alisema msimu wa mwaka wajana NAFRA kulikuwa na matatizo ya upungufu wa magunia na mizani hivyo tatizo hilo aliomba lisijirudie tena msimu huu.

No comments:

Post a Comment