Thursday, May 29, 2014

PAMOJA NA KUMKABA KOO PRFOF. ANNA TIBAIJUKA, LAKINI BAJETI YA WIZARA YAKE IKAPITA

 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka baada ya kuwakilisha bajeti ya Wizara yake ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2014- 2015 Bungeni,ndipo palipotokea waheshimiwa Wabunge wakaanza kuchangia ,ikwa mshikemshike kwa Mhe. Tibaijuka.

Wizara hiyo ni nyeti na  ina mambo mengi na yote yalikuwa na lawama. Wabunge hao walitaja migogoro kibao ikiwemo  wakulima na wafugaji,upimwaji wa viwanja,upatikanaji wa Milki za Ardhi na mengine mengi.

Lakini mwisho wa lawama  kwa waziri huyo Bajeti yake ilipita.Pamoja na lawama kuhusu migogoro inayotokea kila kona ya nchi hii, ifike mahali tusema Prof. Tibaijuka amejitahidi sana katika kuyatatua matatizo ya migogoro ingawa haiwezi kumalizika maana kila kukicha inajitokeza.

Kilichopo ni kwenda kujipanga sawa sasa na watendaji wake,hasa katika utoaji wa Hati milki za Ardhi na Viwanja, wateja wanasumbuliwa kupata hati hizo mtu anaweza kuzungushwa njoo mwezi ujao ,akienda  naambiwa tena njoo baada ya siku 30, basi mradi lugha inabadilishwa hadi kero.Yeye kama yeye hausiki na majaribu hayo yanayo wapata wateja wake.
                                           Prof. Anna Tibaijuka akiwakilisha Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2014 - 2015 Bungeni Mjini Dodoma juzi na kukamilisha jana.

BLOG HUWA JINA, HIVYO BODO NIPO NANINAENDELEA NA KUWASILIANA NA WASOMAJI WA BLOG HII TUPO PAMOJA

Samahani wasomaji wa Blog yanga niliadimika kidogo katika kuwasiliana kwa blog na kupeana habari,Kwa  sasa nipo Dodoma.