Friday, May 6, 2011

KIUMA -BONITA SEKONDARI KUPATA CAPITATION GRAND NA SERIKALI

NAIBU Waziri wa Nchi Elimu TAMISEMI Mhe. Kasimu Majaliwa alimpongeza Mkurugrnzi wa Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi KIUMA DR.M.K.S.Matomora kwa kuanzisha Taasisi mbalimbali katika Wilaya ya Tunduru hasa ya elimu.
Mhe. Majaliwa alisema ni sekondari chache za binafsi zenye kusomesha wanafunzi kwa gharama nafuu za ada,kwa hiyo serikali itafanya utaratibu wa kutoa Ruzuku ya Capitation Grand kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo.

Aidha ameoa wito kwa wananchi walio nje ya nchi kurudi Tanzania kuwekeza katika elimu,wajaribu kuiga mfano wa Dr.Matomora kuacha kazi yake ya Udaktari huko Ujerumani na kurudi kijijini kwake kuanzisha taasisi hizo ili kuinua maendeleo ya ndugu zake katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.Ukiacha Sekondari ya KIUMA  - BONITA,pia KIUMA itakuwa na chuo cha Ualimu

No comments:

Post a Comment