Monday, May 16, 2011

Mchezo wa Vyama vikubwa vyenye nguvu vinawayumbisha wananchi.

VYAMA vya Chama cha Mapinduzi CCM na Chama Cha Maendeleo na Demohrasia CHADEMA,kutokana na kauli za viongozi wa Juu wa Vyama hivyo vinawayumbisha wananchi,kubaini ni nani sasa yuko sahihi.na yupi hayupo sahihi,Wananchi hawajui ninani ataleta maendeleo kwa kila mtu kama ilivyo semwa na inaendelea kusemwa,Utakuta CCM wanasema wanatekeleza Ilani ya Chama chao,CHADEME nao wanaponda utekelezaji huo,hiyo ni nini.Hivyo lengo la vyama hivyo si kumletea mwananchi unafuu wa maisha? Huyu akiwa jukwaani anaponda kivyake,hivyo kwenye vyama hivyo hakuna mipaka ya kumkosoa mwingine hadharani?

Maana kukosoa chama fulani kimeshindwa kufanya vile kwa muda fulani,Na mwingine naye anaponda mbona  wao wamefanya hivi na vile.Hivi hawa wa- Tanzania watasaidhiwa vipi kutokna na mfumuko wa bei hasa Vyakula,vifaa vya ujenzi,pembejeo,nishati na mambo mengine kama mafuta.Tofauti za Itikadi za vyama ndiyo ugomvi,haiwezekani kukaa meza moja kutatua matatizo yanayo wakabili wananchi.Ikishindikana basi kukashifiana majukwaani kupunguzwe watu wamechoka kusikia maneno hayo hayo kila anayesimama majukwaani.

Turejee maandiko ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,hata kama yanawapa kichefuchefu lakini yana maana sana kwa mtu mwenye kutaka kujua nchi hii ilitoka wapi na inakwenda wapi.

No comments:

Post a Comment