Wednesday, May 11, 2011

KIKAO CHA BODI YA BARABARA ZA MKOA WA RUVUMA KUPITIA NA KUPANGA MKAKATI WA MWAKA 2012

Mwenyekiti wa kikao cha bodi ya barabara mkoa wa Ruvuma Mhe.Dkt Christine Ishengoma afungua kikao hicho katika ukumbi wa Songea Club hivi sasa kinacho hudhuriwa na viongozi watendaji wa mkoa,Waheshimiwa Wabunge,Sekta binafsi watumiaji wa barabara,wakuu wa wilaya,wakurugenzi watendaji,wizara ya miundombinu,wahandisi wa wilaya,waalikwa na Sekretarieti ya Mkoa.

Mambo muhimu yatakayo jadiliwa ni pamoja na kupitia utekelezaji wa barabara zinazohudumiwa na TAROADS kuanzia Aprili hadi Oktoba 2010,mpango wa matengenezo ya barabara TANROADS mwaka 2011,Utekelezaji wa matengenezo ya barabara za wilaya kuanzaia Aprili hadi Oktoba 2010 na mpango wa matengenezo ya barabara mwaka 2011na mapendekezo ya matengenezo ya barabara mwaka 2011/2012.

No comments:

Post a Comment