Tuesday, May 10, 2011

MIRADI YA MILLENNIUM CHALLENGE RUVUMA NI KWA UJENZI WA BARABARA ZA LAMI

 Dkt Christine Ishengoma Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akifungua kikao cha ushauri cha Mkoa RCC leo katika ukumbi wa Songea Club.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma  (R P C ) Michael Kamuhanda na Anna Kiwango RSO wajumbe wa kamati ya usalama na ulinzi walikuwepo katika kikao hicho.






MKOA wa Ruvuma umetekeleza miradi ya changamoto ya Millennium challenge kwa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami za Songea  hadi Namtumbo na Peramiho  hadi Mbinga.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt Christine Ishengoma amesema hayo katika hotuba yake ya kufungua kikao cha ushauri cha Mkoa ( RCC ) kilichofanyika katika ukumbi wa Songea Club leo.

Dkt Ishengoma amesema barabara zinazojengwa kwa kiwango cha lami ni pamoja na ya Songea hadi Namtumbo yenye urefu wa kilometer 67 inayojengwa na kampuni  ya Sogea – Satom kwa mkataba wa miezi 27 na Peramiho hadi Mbinga inayojengwa na kampuni ya Sinohydro Corporation  Ltd yenye urefu wa kilometa 78.kwa mkataba wa miezi 27.

Na nyingine ni ya Namtumbo hadi Tunduru yenye urefu wa kilomita 193 mkandarasi ni M/S Progressive Higleig,JV ameanza maandalizi kwa kuleta mitambo.

Aidha alisema kuwa mkoa umelenga kuzalisha Tani 1,257,046  za mazao kati ya hizo Tani 107,882 za mazao ya biashara na Tani 1,149,164 mazao ya chakula,hii ni alama ya kazi kubwa inayofanywa na wakulima za Ruvuma wanastahili pongezi kubwa.

Dkt Ishengoma ametoa wito kwa halmashauri kuhimiza wananchi kujipanga kwa ajili ya musimu ujao wa kilimo kwa utambuzi wa upangaji wa pembejeo za ruzuku na matumizi ya power tiller  badala ya jembe la mkono.

Kuhusu huduma za jamii alisema sekata ya elimu haikufanya vizuri mwaka uliyo pita hivyo kujibanga upya ili kuinua kiwango cha ufaulu,huduma ya umeme alisema zi mzuri katika Manispaa ya Songea ,hali itakuwa nzuri baada ya kupata Gridi ya taifa hapo Desemba 2013.

Katika hotuba yake Dkt alisema anachukizwa sana na waharibifu wa mazingira kwa kukata miti,kuchoma mkaa bila vibali na kilimo cha kuhama hama,inabidi sheria ndogo  ziwekwe za kuhifadhi mazingira katika Halmashauri zote mkoani.huo.

No comments:

Post a Comment