Saturday, April 30, 2011

MAMA WA CATHERINE MWIKWA KWENYE SEND - OFF SONGEA CLUB

 Mama mzaa chema mzaa Catherine Mwikwa akitoa  shukrani,kwa wageni na mawaiza mazuri kwa Catherine na mmewe kuwa wafuate mwenendo mzuru wa maisha wa mme na mke.Bibi Doral Mwikwa amemtaka Catherine awe mama wa mfano hapo baadaye.
 Bibi Doral Mwikwa akionyesha baadhi ya vyombo alivyo pewa binti yake kama zawadi baadhi ya zawadi ni sofa,dressiing table,tv table dinner sets and somany things.
 Akina mama kwenye vikundi vyao wakiingia na zawadi za kufupa wakaanzie maisha yeye na mume wake.
 Catherine akimpa mzazi wa kiume keki kwa heshima kubwa kabisa kwa kupiga magoti.
High table ya wazazi wa kike. 

SEND OFF YA CATHERINE MWIKWA YA AINA YAKE SONGEA CLUB

 Sen - Off ya Binti Leopord Mwikwa Catherine Mwikwa kulia wakiingia katika ukumbi wa Songea Club jana.
 Catherine na Mme wake baada ya kuingia ukumbini Songea Club Songea
 Catherine akikata keki ili alishe mmewe wazazi na wageni waalikwa.
 Catherine apeleka keki kwa mwenyekiti wa kamati ya sherehe Songea Club.
 Mama mzazi wa Catherine apewa zawadi na wanawake wenzake wa kwenye vikundi vyake Bibi Dikoral Mwikwa katika Ukumbi wa Songea Club jana.
Catherine akimlisha Dr.Tonya kwa niaba ya marehemu Baba yake Leopord Mwikwa ambaye alisimama kama mzazi upande wa kike.Send - off hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya watu 700.

ILO YAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KURDHIA BIKATABA YA USALAMA NA AFYA KAZINI

Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani Bwana Magnus Minja akisoma hotuba ya Bwana Alexio Musindo,Mkurugenzi wa ILO Ofisi ya Tanznaia,Kenya ,Uganda na Rwanda  wakati wa maadhimisho ya usalama na afya kazini tarehe 28 mwezi huu Songea Mkoa wa Ruvuma


SHIRIKA la kazi Duniani ( ILO ) laipongeza serikali ya Tanzania kwa kuwa tayari na sheria ya usalama na afya kazini mwaka 2003 ambapo mikakati inaendelea ya uhakiki wa utekelezaji wake.

Mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani Bwana magnus Minja alisema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya usalama na afya kazini kilichofanyika mkoani Ruvuma tarehe 28 mwezi huu.

Bw.Magnus alisema kuwa Tanzania imekwisharidhia baadhi ya mikataba inayohusiana na usalama na afya kazini ambayo ni mikataba Na..148 wa mwaka 1977 unaohusu mazingira ya kazi,Na.152 wa mwaka 1979 unaohusu usalama na afya kazini,kazi za bandarini na ule wa  Na.170 wa mwaka 1990 unaohusu matumizi ya kemikali.

Alisema ni matarajio ya Shirika hilo kuwa juhudi za serikali na wadau wengine wataendelea kuchukua jitihada zaidi ili kuridhia mikataba mingine iliyobakia ukiwemo mkataba Na.187 wa mwaka 2006.Pamoja kuwepo kwa masharti ya usalama kazini hasa kwenye makampuni makubwa,pia kuyasaidia makampuni madogo katika utekelezaji wake kwa vitendo.

Thursday, April 28, 2011

RAHA YA NDOA NI KUKAA PAMOJA MME NA MKE KUKAA PAMOJA KUPANGA MIKAKATI

Inapendeza kweli kweli kama Wana - Ndoa wakiwa pamoja katika kupanga mikakati ya kuendeleza miradi yao ,sehemu ya kazi ambapo leo Manispaa ya Songea wananchi wake wameadhimisha sherehe za usalama na afya kazini.Kama Blog hii ilipowakuta Mr& Mrs gaston Chembele ofisini kwao leo.
Ofisi yao ipo mkabala na Benki ya NMB Songea na Soko kuu,wauzaji wa pikipiki za MWADA Jet Fighter zenye nguvu na nzuri kwa yebo yebo.

BAADHI WAJITOKEZA KUPIMA UKIMWI KWA HIYARI KATIKA BANDA LA USHAURI NASAHA SONGEA LEO

Baadhi ya wafanyakazi na wananchi wa Manispaa ya Songea wakiwa katika foleni ya kwenda kupima UKIMWI kwa hiyari kwenye banda la ushauri nasaha katika maadhimisho ya usalama na afya kazini leo katika uwanja wa majimaji Manispaa ya Songea leo.

SERIKALI ITOE VIFAA VYA KINGA KAZINI KUEPUSHA AJALI MGAYA

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bwana Nicholaus Mgaya  asema serikali,waajiri na wafanyakazi wazingatie sheria zilizoainishwa na Shirika la kazi Duniani 
(ILO ) za usalama na afya kazini ili kupunguza ajali na magonjwa yanayo tokea sehemu za kazi.

Bw.Mgaya alisema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini kitaifa zilizofanyika Mkoani Ruvuma katika manispaa ya Songea uwanja wa maji maji leo.

Aidha alisema ni muhimu serikali  na waajiri kuwa na vifaa vya kinga za ajali kazini na kutoa elimu  na mafunzo sehemu za kazi.

VIKOMBE VYA MWAGWA KWA WASHINDI WA USALAMA NA AFYA KAZINI SONGEA UNGNA NAMI UJIONEE

Waziri wa kazi na Ajira Mhe.Gaudensia kabaka akimkabidhi mshindi wa jumla Bwana Isack Senya wa Safety Superintendent baada ya kufunga maadhimisho ya usalama na afya kazini katika uwanja wa majimaji Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma

 Hivyo ni vikombe ambavyo Waziri amevigawa kwa makampuni yaliyoshinda katika usalama na afya kazini katika maadhimisho ya usalama na afya kazini, ambapo Shirika la Kazi Duniani (ILO) limeungana na Serikali ya Tanzania,waajiri na wafanyakazi Duniani leo.

SHIRIKA LA KAZI DUNIANI ILO LAUNGANA NA SERIKALI YA TANZANIA LEO KATIKA MAADHIMISHO YA USALAMA NA AFYA KAZINI SONGEA RUVUMA

Mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani ( ILO ) Bwana Magunus Minja akitoa maelezo ya malengo ya Shirika hilo kwa usalama na afya kazini ili kuepusha ajali na vifo kwa wafanyakazi Duniani.


MAADHIMISHO ya siku ya Usalama na Afya kazini Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Majimaji katika Manispaa ya Songea,Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa Gaudensia Kabaka ,baada ya kufunga maadhisho hayo alitoa zawadi katika taasisi 9 zilizo dhibiti viashiria vya usalama katika kazini.

  Mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani Bwana Magunusi Mijna alisema,  Serikali ya Tanzania leo imeungana na Shirika la Kazi Duniani ( ILO) waajiri,na awafanyakazi  pamoja na vyama vyao vinavyo simamia utamaduni wa usalama na afya sehemu za kazi,yenye kauli mbiu “ Usimamizi wa usalama na afya: Zana ya uboreshaji endelevu”

Bwa.Minja alisema kuwa mwaka huu tunaadhimisha miaka 92 ya ILO kushughulikia haki katika jamii,kulinda  maisha na afya ya wafanyakazi wote ikiwa ni sehemu ya lengo pana la ILO la kazi yenye staha sehemu za kazi.

Alisema kwa kunukuu kuwa “Kulingana na azimio la Seoul la mwaka 2008 kuwa utamaduni wa taifa wa kulinda usalama na afya ni ule ambapo haki ya usalama na afya kazini inaheshimiwa katika ngazi zote,ambapo serikali ,waajiri, na wafanyakazi wanashiriki kikamilifu katika kufanikisha mazingira hayo.

Bw.Minja alisisitiza kuwa kazi isiyo salama ni janga  la binadamu,ambayo husababisha  ajali,magonjwa na kupunguza uwezo wa kufanya kazi na kufupisha maisha ya mfanyakazi.Ambapo kila mwaka mamilioni ya majanga hutokea bilia kuripotiwa.

  Aidha alisema ili mfanya kazi awe salama mahali pa kazi ni budi kufuata mifumo ya  ( OSHMS ),kwa kuzingatia na  kuandaa Sera ya taifa ya usalama kazini  na kuweka miundombinu ya utekelezaji wa Sera na Programu zilizoandaliwa ,Programu ya taifa ya usalama na afya kazini kwa kuwa na  malengo ya kitaifa kwa muda uliyo pangwa.

Alisema ingawa ajali haina kinga lakini tahadhari ni muhimu kuchukuliwa na mfanyakazi mwenyewe panapo tokea viashiria vya hatari sehemu ya kazi,kutoa elimu na mafunzo ana kuzingatia sheria zilizowekwa na  Serikali, vyama vya wafanyakazi,waajiri wafanyakazi na mashirika ya kijamii,ili kazi isiwe ya kufupisha maisha bali iwaongezee maisha wafayakazi.

WAZIRI WA KAZI NA AJIRA MHE.GAUDENSIA KABAKA AHUTUBIA SONGEA LEO

 Waziri wa Kazi na Ajira Mhe.Gaudensia kabaka akihutubia maelfu ya wafanyakazi katika uwanja wa majimaji  Katika Manispaa ya Songea leo katika kilele cha maadhimisho ya 8 ya usalama na afya kazini
 Waziri katika  picha ya pamoja na baadhi ya wafanya kazi





Waziri na vikombe kabl haja kabidhi kwa washindi  hapo chini.
W
 Waziri akimkabidhi kikombe cha ushindi wa jumla Bw.Isack Senya

Ajali kazini husababisha hasara na kupunguza uzalishaji – Kabaka

KILA mwaka serikali imekuwa ikipoteza wafanyakazi wake kwa kupoteza maisha au sehemu za viungo vyao vya mwili katika sehemu zao za kazi pengine bila ya kuwa na taarifa kutoka kwa wa waajiri,vyama vya wafanyakazi kwa kutokuwa na takwimu za watu walioathirika  mahali pa kazi.

Waziri wa kazi na Ajira  Mhe. Gaudensia Kabaka alisema hayo siku ya maadhimisho ya 8 ya usalama na afya kazini yaliyo fanyika kitaifa Mjini Songea katika uwanja wa majimaji leo.

Mhe.Kabaka alisema Serikali,waajiri na wafanya kazi pamoja na vyama vya wafanyakazi  lazima kuzingatia kanuni zilizo wekwa na Shirika la Kazi Duniani ( ILO ) la kuwa na sheria zitakazofuatwa. Za usalama na afya kazini.

Alisema ukiona watu hawaendi kazini kila mara ujuwe sehemu hiyo si salama,hivyo kuwe na kanuni na sheria zitakazo fuatwa na kila mfanya kazi na kuwa na vifaa vya kujikinga na ajali hasa sehemu za ujenzi,migodi na kwenye viwanda.ili kupunguza ajali.

Baada ya kufunga maadhimisho hayo Mhe.Kabaka aligawa zawadi kwenye makampuni tisa ambayo yameonyesha umahili wao katika usalama na afya kazini ,zawadi hizo likuwemo vikombe pamoja na vyeti.

Monday, April 25, 2011

Sisi ni Wanzibar na wao ni Wanzibara- Muasisi wa Muungano Mwalimu Julius Nyerere

 Maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni matokeo ya wasisi wa Muungano huo Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Amani Abed Karume tarehe 26 Aprili 1964.
Huwezi Kuutenga Muungano,kufanya hivyo ni dhambi kubwa,lakini kuna watu wenye mitazamo yao wanataka kuuvunja Muungano huo ambao umewaunganisha wananchi wa Tanganyika na Zanzibar.Tujaribu kurejea hotuba za Baba wa Taifa Mwl. Nyerere.

AMIRI MKUU WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA DKT KIKWETE MGENI RASMII MIAKA 47 YA MUUNGANO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri mkuu  wa vikosi vya ulinzi na usalama Dkt Jakaya  Kikwete atakuwa Mgeni Rasmi katika kilele Muungano wa Tanganyika na zanzibar, Tarehe 26 Aprili 2011 kwenye uwanaja wa Amani Mjini Zanzibar.

BLOG YA TUJIFUNZE KUSINI INAWA WATAKIA WATANZANIA WOTE SIKUKU NJEMA YA MIAKA 47 YA MUUNGANO

Tarehe 26 Aprili 2011 Tanzania inaadhimisha miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa tarehe 26 Aprili 1964 kwa yaliyokuwa mataifa mawili.Hongera  Wa - Tanzania kwa kudumisha muungano huo.

JUMA TATU YA PASAKA , NILITEMBELEA KUONA RELI YA KATI YA DAR ES SALAAM HADI KIGOMA NILIONA KAMA HIVYOO!!1

 Hapa ni Dodoma Railway Station ukiangalia mbele yako Train inaelekea kigoma,Ukweli miundo mbinu ya Shirika hili ni mibaya ndiyo maana ajali nyungi zinatokea kila mara katika Reli ya kati kwa sababu reli hii imesahaulika hakuna usafi ,hakuna uangalizi wa kuchunguza mataluma yaliyo tolewa na wahujumu wa mali ya umma.
Hapa Reli hii inaelekea Dar es salaam ona ilivyo kuwa na nyasi nyingi ,sasa hapa ni mjini Dodoma je huko katikati ya safari kama vile Zuzu, Malampaka,na sehemu nyingine kukoje,tatizo yale magenge ya wafanya kazi wa Reli hayapo tena.Serikali inusuru Reli hii kwa kuwa ni kiungo pekee cha safirisha mizigo kwenda nchi jirani.

Sunday, April 24, 2011

WATAALAMU WA KUCHIMBA NA KUSAFISHA SEHEMU NYAO FOOT PRINT LAITONI ARUSHA ZINAENDELEA

 Huyu kiumbe aliyeishi Laitoni Arusha nyayo zao zipo Laitoni zimehifadhiwa kitaalamu na sasa zimekuwa kivutio na chanzo cha ingizia fedha za kigeni kwa shughuli za utalii.
 Hayo ni mafuvu ya viumbe hao ambao inasemekana kuwa hawakuwa na lungha ila walikuwa wakitoa sauti tu
 Mtangazaji wa TBC akihojiana na mtaalamu wa mambo ya kale katika kijiji cha laitoni,akisema vijana wa kimasai wamefundishwa jinsi ya kupokea na kutembeza watalii.Alisema serikali kwa kushirikiana Wizara ya Utalii na maliasili na Ujenzi zimeweka miundo mbinu ya barabara kuwa bora ya kupitika majira yote ya mwaka.
Wataalamu wa nje na wandani ya nchi wakisafisha nyao ( foot Print ) za Binadamu wa kwanza aliyeishi eneo hilo la kihistoria Laitoni Jijini Arusha - Tanzania.

Nyimbo za kumsifu bwana zilisikika katika Ibada ya Pasaka makole Dodoma leo


Blog hii inaungana na wakristo wote duniani kuadhimisha kifo na kufufuka kwake Yesu Kristo kwa Ibada na nyimbo kama hivyo

Mtaalamu  wa nota katika muziki akikolezea kwaya ya Parokia ya Makole siku ya Pasaka leo Manispaa ya Dodoma.
l
 Picha ya pamoja ya wanakwaya hawa wakati wakiimba ule wimbo wa Aleluya bwana amefufuka aleluya.
Wana - kwaya hao wakitoka nje baada ya Ibada ya kwanza kanisani hapo.

Nyoka na sifa zao Dr.Victor Mwafongo

 Dokta Victor Mwafongo anachanganua aina za nyoka.Alitaja kuwa ni pamoja na nyoka wa :-
  • Wa shimoni
  • Miti  
  • Baharini
  • Misitu
Wapo wenye sumu kali kama green mamba ( Cobra ) wenye sumu wana meno marefu ya juu,wale wenye meno madogo madogomadogo hawana sumu.

Wale watu wanaochezea nyoka kuwa wanawatoa meno ndipo wanacheza nao nyoka hao haijalisha anasumu au laa.

UFUFUKO WA YESU KRISTU ULETE AMANI,UMOJANA NA MSHIKAMANO MIONGONI MWA WATANZANIA

 Heri ya pasaka kwa watu wote Duniani kwaa  wanao mwamini na wasio mwamini,Padre Adam Mbando wa Parokia ya Makole Manispaa ya Dodoma akiwa mbele ya Altare akisubiri vipaji.' Ufufuko wa Yesu Kristo ni ishara ya uko mbozi wa binadamu wenye dhambi,hivyo watu wazidi kusali sana ili kuiombea nchi yetu maana kunajitokeza matendo yanayoonyesha uvunjifu wa amani' Alisema Padre Mbando.
 Aleluye Bwana amefufuka,aleluya imeenea duniani kote kwa watu wenye mapenzi mema.Padre Adam mbando wa Parokia ya Makole Manispaa ya Dodoma,Amesema watu wanatakiwa wafufuke na Bwana wetu Yesu Kristo.Alisema Baadhi ya Wa- tanzania wanataka kuharibu kisiwa chetu cha Amani cha Tanzania.
Amani ikikosekana ubinadamu unapungua,Yesu Kristo aliteswa kisha akafa,siku ya tatu alifufuka,kuonyesha utukufu wake,na hakuna ufufuko bila ya kifo,na hakuna kalvari bila ya kuteswa.Na umaskini wa watanzania sio ni laana tuliyopewa na Mungu,hapana bali ni ukosefu wa uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo, kwa wale waliopewa dhamana ya kuongoza nchi.
 
 Kwaya ya Mtakatifu Kaloli lwanga iliyo kolezea Ibada ya Pasaka ya asubuhi katika kanisa la parokia ya Makole katika Manispaa ya Dodoma na Mkesha wa Pasaka.
Honhera zao wanakwaya hao Mungu awabariki wazidi kukoleza katika Ibada mbalimbali katika Parokia ya Makole.

SIKUKUU ZINA MAMBO YAKE ILIKUWA HIVI JUMAMOSI KUU ONE WAY MJINI DODOMA

Hekaheka za maandalizi ya sikukuu ya Pasaka zilikuwa zikijitokeza kila uendapo katika Manispaa ya Dodoma Jumamosi Kuu,watu walikuwa wakitafuta mahitaji kwa ajili ya Pasaka.Lakini kutokana na umati wa watu katika mitaa ambayo ni mifinyu kwa ajili ya watu na magari na pikipiki,Dereva wa Taxi  ambaye alikuwa nyingi asubuhi subuhi alijikuta anamkwaruza mwendesha pikipiki.Ikawa pata shika washukuru Mungu Trafic hawakutokea.

Pombe hizi jamani zinaleta mambo hasa wakati huu wa sikukuu,Serikali inashauri waendesha vyombo vya moto wawe makini siku hizo,na wasiwe nyingi wakiwepo barabarani lakini haisaidii.Tufanye nini kuepuka ajali?

Friday, April 22, 2011

LEO IJUMAA KUU !11 NAWATAKIA WA KRISTO WOTE DUNIANI IJUMAA KUU,NA KUWA TAKIA PASAKA NJEMA

Ni siku pekee kwa wakristo kukumbuka siku ambayo Yesu Kristo anakamatwa na kuteswa kisha kutundikwa Msalabani kwa ajili ya dhambi za wanadamu baada ya Adamu na Hawa kukiuka maagizo waliyopewa na Mungu.

Wednesday, April 20, 2011

HABARI KWA UFUPI KITENGO CHA HABARI,ELIMU NA MAWASILIANO KUANDAA TOLEO MAALUMU ARINE MOROGORO

 Ni siku ya kwanza kabisa baada ya wajumbe wote kuwasili katika hotel ya Arine Inn eneo la Kola hill Morogoro.
 Kitengo cha Habari ,Elimu na Mawasiliano na Wahariri wa Jarida la  Elimu Tanzania (Ed- SDP ) wa kanda saba za Elimu Tanzania huwa wakikutana kuandaa Jarida hilo  Mkoani Morogoro ili kuandika mambo muhimu kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.Wakwanza ni Mhariri wa Moshi kilimanjaro na Oliva kato wa Kitango cha habari wakiandika habari.
 Mhariri Mstaafu wa tabora Bwana Lucas Ndanga wa kwanza na Kaimu Mhariri wa Morogoro Bwana Jems Tem wakiwa katika kuandika habari.
 Baandaa ya kuchambua na kuandika habari hizo zimepelekwa kwenye Computer kwa Lyaout ambapo Dada Oliva kato akiwa kwenye Computer,Mratibu Msaidizi Bwana Ntambi Buyanzu,akisoma kwa masahihisho ambapoElizabeth Pangras mwenye bauni lenye maua akihakiki.
 Wahudumu wa Hotel hii wakiwa tayari kwa  mahanjumati kwa wanahabari hao baada ya kazi maalumu
Hapa na mie nikiwa na wanahabari wenzangu tukitoka Arine Inn kuelekea tulikofikia hapa Mjini morogoro

Thursday, April 14, 2011

WANANCHI WA MKOA WA RUVUMA WAMEPOTEZA TUMAINI YA KUONA SOKA TENA

Wapenzi wa soka wa ndani na nje ya mkoa wa Ruvuma wamepoteza tumaini ya kuona soka katika uwanja wa majimaji ( Wa- na lizombe ) baada ya Timu hiyo kushuka daraja.

Sijui alaumiwe nani katika kushuka Daraja Timu ya Majimaji,Ulaumiwe uongozi wa serikali ya mkoa?,wanaoongoza timu hiyo?,usajili mbaya wa wachezaji?,huduma mbovu kwa wachezaji hao?.hakuna wafadhili wa timu hiyo?.

Hebu wenzetu walio nje ya mkoa wa Ruvuma wenye uwezo kusaidia timu hiyo ili kurudisha hadhi yake kama miaka  ya 70.


Wednesday, April 13, 2011

HONGERA SERIKALI YA MKOA WA MOROGORO KUJENGA SEKONDARI YA UKUMBOSHO WA SOKOINE

Naipongeza Serikali ya mkoa wa Morogoro kushirikiana na Wilaya ya Mvomero kuandaa Bilioni 12 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari itakayo pewa jina la Sokoine Memorial High Secondary School eneo alilofia aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine Wami Ruhinda.

Sekondari ya kidato cha tano na sita itakyo sajili wanafunzi kutoka mikoa yote nchini.Ni vyema basi na Serikali za mikoa mingine Tanzania kuiga mfano huo mzuri ulio fanywa na Serikali ya Mkoa wa Morogoro kufanya kitu cha ukumbusho wa maisha.

Cha ajabu na cha kushangaza kuna baadhi ya viongozi mashuhuri katika mikoa fulani walionyesha juhudi zao katika uongozi na Mungu amewaita mbele za haki hawakufanyiwa kama ilivyo fanya Serikali ya Mkoa wa Morogoro.

Mfano mzuri na rahisi sana, Aliyekuwa Mbunge wa Songea Mjini Hayati Raurence Mtazama Gama ,Alifanya mambo mengi ya maendeleo katika mkoa wa Ruvuma,hadi leo wanasua sua kumpatia kitu chochote jina kama kumbu kumbu Mzee Gama.


Kuna shule ya sekondari inayojengwa Wilaya ya Namtumbo ya kidato cha tano na sita inayojengwa kwa ushirikiano wa wilaya zote za mkoa wa Ruvuma,Afisa Elimu wa mkoa huo alipendekeza sekondari hiyo iitwe Jina la Gama kumuenzi kutokana na juhudi alizozionyesha wakati alivyo kuwa mkuu wa mkoa huo,kilicho tokea huwezi kuamini baadhi ya wabunge alikataa kata kata kupewa sekondari hiyi jina la Gama. Makubwa wenyewe kwa wenyewe wanakataana.


DUNIANI KUNA MAMBO KWELI JAMANI TOKA LINI MAREHEMU ANAPOKEA MISHAHARA ?

Ukaguzi wa mahesabu ya fedha za serikali imebaini Halmashuri zetu zimejihusisha na malipo hewa.Malipo yaliyolipwa ni ya mishahara.Kinacho shangaza na haiingii akilini ya kumlipa mshahara marehemu.Inamana marehemu hao wanatoka kaburini kwenda benki kuchukua fedha?

Huwezi kuamini marehemu wa dizaini hiyo wanakwenda benki kukopa fedha,lakini mfanyakazi aliye hai akienda kuonana na meneja wa mikopo katika benki hizo hapati kwa urahisi,lakini marehemu wanapata mikopo hiyo kwa ulaini.

Lakini kila mwaka watumishi wa Umma wanajaza fomu za kuhakikisha au kuhakiki malipo ya mishahara hewa,inamana Halmashauri hizo zilizokubwa na ulipaji mishahara  hewa, huwa wanapeleka wapi fomu za uhakiki wa malipo hewa ya mishahara?

NI KWELI USEMI HUU,MTU ANA VIDOLE 11 VYA MKONO?

Kuhakikisha kuwa mtu ana vidole 11,hebu hesabu vidole vyako kuanzia kidole gumba hadi cha meisho kama hivi. 10,9,8,7,6 + 5  =  11 Je unakubaliana na kubaliana na theory hii? Hii inathibitisha kuwa wa kwanza anaweza kuwa wa mwishi na wamwisho akawa wa kwanza.

KUMBE SOKWE NAO WANA UTAWLA?

Hifadhi ya Taifa ya Gombe ni kivutio kikubwa sana kwa watalii,Hifadhi hiyo  ina Sokwe ambao wana utawala wa kuachiana.Kwa  mujibu wa wakuu wa hifadhi hiyo ni kwamba kiongozi wa sasa wa Sokwe hao ni mkali sana.Inasemekana kuwa aliwahi kujamiiana na mama yake hivyo aliugua sana.

Aidha sokwe akiugua wanatabia ya kujitafutia dawa ya majani au mizizi,wakitumia dawa hizo wanapona.Sokwe hao wanapenda kuwa karibu na binadamu.Karibu Tanzania ukajionee maajabu ya vivutio mbalimbali.