Sunday, December 18, 2011

MKUU WA MKOA WA LINDI MHESHIMIWA LUDOVICKI MWANANZILA AYASHUTIA MALORI YANAYOSOMBA JASI ( MAWE YA CHOKAA ) WILAYANI KIWLA BILA KULIPIA MAPATO HALM,ASHAURI

 Lori lililokutwa na mpigapicha wa blog hii wilayani kilwa kijiji cha Manadawa taika mkoa wa Lindi likiwa na shehene ya mawe ya chokaa yakipeleka katika kiwanda cha saruji,Wazo Hill kama malighafi katika kiwanda hicho.
 Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Ludovick Mwananzila, katika siku tofauti katika ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Kilwa, aliwaambia wananchi na uongozi wa wilaya hiyo kuwa macho na maliasili walizo nazo,na kwamba kama mali hizo zinachukuliwa basi zichukuliwe kihalali,Ha;mashauri ipate mapato yake kutokana na mali iliyopo katika halmashauri.
Alisema malori kwa malori yanachukua mawe ya chokaa bila  ya kulipia mapato katika halmashuri alisema tani moja ya mawe hayo ni Tshs.80,000/= na kwa siku ni tani ngapi zinachukuliwa,ni kiasi gani cha pesa halmashauri kinapoteza,aliwahimiza kuwa halmashauri iwatoze ushuru wa kuchukua malighafi hizo.

No comments:

Post a Comment