Thursday, February 14, 2013

HUDUMA ZA UHAMIAJI MKOANI RUVUMA ZINATIA FORA KWA WATEJA WAKE

 Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Bw.Shaaban Omar mwenye miwani ankiwa na Mhariri  Msaidizi wa TUJIFUNZE Kanda ya Kusini Bw.Juma Nyumayo wakiwa kwenye Mtandao wa Internet katika ofisi ya Uhamiaji Mkoa leo.
Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma Bw.Shaaban Omar mwenye suti nyeusi akizungumza na Mhariri wa TUJIFUNZE Kanda ya Kusini Bw.Christian Sikapundwa katika ofisi ya Uhamiaji leo Mjini Songea.



NAIBU Afisa uhamiaji wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Shaaban Omar amethibitisha hayo ofisini kwake leo alipotembelewa na Blog hii kutaka kuelewa shughuli zao katika kuhudumia wananchi na wageni kutoka nje ya nchi.

Bw. Omar amesema ofisi yao inajitahidi kuhudumia wateja wanao kwenda kuhitaji huduma zao.

Ametaja huduma ambazo wanazitoa ni pamoja na  kutoa hati za kusafiria ( Pass Port ).kutoa Visa kwa wageni,kutoa hati za muda mfupi kwa wageni ambao watahitaji kufanya shughuli zao zikiwemo za kufanya kazi za kijamii,kuanzisha mchakato wa utoaji wa Uraia, ambapo katika utoaji wa vitambulisho vya taifa wao ni wadau.katika masuala ya upatikanaji wa vitambulisho vya taifa vya Uraia.

No comments:

Post a Comment