Monday, February 18, 2013

DKT SHUKURU KAWAMBWA ATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 789 WAFUTIWA MATOKEO YAO

 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Dkt Shukuru Kawambwa leo ametangaza matokeo ya kidato cha nne,amesema matokeo ya ni mabaya sana ikilinganishwa na matokeo ya nyuma. Hasa kwa masomo ya sayansi sababu shule nyingi za vijijini hazina maabara wala walimu wa kufundisha masomo hayo.
Aidha Mhe.Kawambwa amesema wanafunzi 789 wamefutiwa matokeo yao kati ya hao 624 wa shule za serikali na wanafunzi 148 wa kujitegemea na 17 wa wanaojiandaa kwa mitihani.kwa sababu ya udanganyifu wengine wemeingia katika chmba cha mitihani na madaftari na waliyoshindwa kabisa kujibu maswali katika mitihani hiyo waliamua kujaza matusi.
Sasa ninani wa kulaumiwa?,wanafunzi,wazazi ,walimu,au viongozi wa Elimu? Tutafakari sana kuhusu hilo,sekondari ni nyingi na matokeo mabaya ni mengi vilevile,ni elimu au bora elimu? ni wakati wa kubangua bongo watanzania kila kona ni matatizo lukuki.

No comments:

Post a Comment