Friday, February 8, 2013

MITAALA YA ELIMU TANZANIA IMEBORESHWA SI ZAIDI YA MARA TANO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Paul S. D. Mushi Kifafanua jinsi maboresho ya Mitaala ya Elimu ilivyo yalivyfanyika kwa Maafisa na wadau wa Elimu Mkoani Ruvuma hivi karibuni.


KWA mujibu wa  Kurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Paul S. D. Mushi alisema Maboresho ya pili yalitokea baada ya miaka sita ili kuingiza mapendekezo ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea mwaka 1967 katika mitaala na miaka 12 baadaye.Benki ya Dunia ilipendekeza kuanzishwa kwa Michapuo ya Ufundi,Kilimo na Biashara mwaka 1979 ambapo mitaala hiyo ilianzishwa.

Alisema mwaka 1982, Kamisheni ya Rais ilitoa mapendekezo ya kuboresha Mitaala,baada ya utafiti wanchi nzima chini ya Tume ya Makweta na maboresho ya katekelezwa kati ya miaka ya 1992 na 1997 ambapo baadhi ya masomo  na mada vilipunguzwa na mtaala kuboresha ili kwenda na wakati.

Aidha Dkt Mushi alisisitiza kuwa madiliko makubwa ya Kisekta yalitokea baada ya hapo na  wataalam wengi walishiriki kutoa mapendekezo ya Mpango kabambe wa Elimu mwaka 1999 na Mpango wa Kisekta wa Maendeleo ya Elimu wa mwaka 1999 – 2009.

Alisema kuwa kuzaliwa kwa Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi ( MMEM 2000-2006) ukafuatiwa na Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari  ( MMES 2004 2009 ), ambavyo vilielekeza maboresho ya elimu ya awali ,msingi, sekondari na  ualimu kati ya mwaka 2003 na 2004 hadi mwaka 2007 na 2008.

Alisema Taasisi  ya Elimu Tanzania iliongoza maboresho yote ya mitaala kuanzia ilivyo undwa mwaka 1964  na ilikuwa ilipokea malalamiko ya wadau hasa walimu kutoridhishwa na mchakato wa maboresho hayo .na kwamba walimu hao walihitaji mafunzo kuhusu namna ya kutekeleza mitaala iliyoboreshwa.

Na Taasisi hiyo imeridhia kwa kutoa mafunzo kwa kuwafuata walengwa waliko ili kuipunguzia serikali gharama na ,lengwa watagharimia vitini vya kujifunzia,TET itafika kokote pale walengwa walipo kutoa mafunzo ya maboresho ya  mitaala hiyo.

No comments:

Post a Comment