Wakuu wa shule za sekondari za Mashujaa na Mazoezi Matogoro wakileza jinsi wanafunzi wa kidato cha kwanza wanavyo ripoti kwa kusua sua hadi sasa.Mwenye kaunda suti nyeusi kushoto ni Bw.Leonard Matao wa Shule ya sekondari Mashujaa na wa kulia mwenye shati nyekundu ni Mkuu wa shule Mazoezi Matogoro Bw. Marianusi A. Komba.
Bw.Marianus A,Komba
Bw.Leonard Matao
BAADHI ya wakuu wa shule za
sekondari katika Manispaa ya Songea wamekanusha
kuwepo kwa utitili wa michango katika shule zao za sekondari.wamesema
kuwa michango ambayo inachangishwa ni michango ambayo inasaidia kuendesha
shule.
Wamesema kuwa Serikali haipeleki
fedha ambazo zingilipwa kwa kila mtoto kusaidia wazazi na walezi kama
walivyopanga,hivyo kamati ya shule na wazazi na walezi wanakubaliana
kuchangisha fedha ili kuziba mapengo ambayo serikali ilipaswa kuchangia kwa
kila mtoto kama ilivyo ahidi.
Kuhusu watoto kutoripoti shule
wale waliyochaguliwa kuingia kidato cha kwanza , Mkuu wa shule ya sekondari Mazoezi Matogoro Bw.Marianus A.
Komba na Mkuu wa shule Mashujaa Bw.Leonard Matao wanasema ni kweli kwamba bado
kuripoti kwa wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza hakuridhishi.
Hivyo wakuu hao wanaungana na tamko la Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma kuwa wazazi na walezi kuwapeleke watoto
wao shule kabla ya tarehe 01/03/2013 aliyo sema mkuu wa mkoa huyo,
No comments:
Post a Comment