Tuesday, February 12, 2013

UAMUZI WA KUJIUZURU UPAPA ,PAPA BENEDICT KWA UMRI WA MIAKA 85 NI WA BUSARA SANA KWA KANISA NA KWA WAUMINI WAKE

Uamuzi wa Papa kutangaza kwake kutaka kujiuzuru ifikapo saa sita usiku wa tarehe 28 mwaka huu ni wa busara sana kwa Kanisa na kwa waumini wa kanisa hilo.
Papa amesema kuwa umri wa miaka 85 aliyokuwa nayo inatosha katika kutoa huduma kwa kanisa hilo,ameona ni vyema aachie ngazi apishe mwingine aendeleze Utume huo ambaye atakuwa na nguvu na afya ya kutosha katika Utume huo.
Wapembuzi wa mambo wanajaribu kuangalia nani atakuwa mrithi wake,kutoka Barani Ulaya,Marekani ya Kaskazini au barani Afrika.
Uwezekano ukawepo Bara la Amerika na Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya waumini wa Kanisa hilo la Roman Catholic.Yote tuna mwachia Mungu kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu kwa Makadlnali watako kutana kwa kazi hiyo.

Ambapo ishara ya moshi huo wa kuonyesha sala  na maombi ya kumpata Papa mpya yamekubalika,Sala na maombezi ya waumini hao Duniani kutasaidia kazi hiyo kuwa nyepesi.

No comments:

Post a Comment