Wednesday, February 27, 2013

MHE. BALOZI KHAMIS KAGASHEKI ATAKA MAKUMBSHO YA TAIFA YA MAJIMAJI SONGEA YATUNZWE ILI KUVUTIA WATALII


 Picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Hkamis Kagasheki  wa kwanza kulia mwenye kitambaa cheupe,wakatikati ni mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabit Mwambungu na tatu kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera kwenye makumbusho ya Taifa ya Majimaji Manispaa ya Songea leo.

 Picha ya pamoja na wazee wa mila wa makumbusho ya majimaji

 Picha ya pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Ruvuma waliyo simama nyuma.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Kagasheki ametaka Makumbusho ya Taifa ya Majimaji katika Manispaa ya Songea yatunzwe yawe katika hali ya usafi ili yawe kivutio kwa watalii ambao watatembelea makumbusho hayo kusini mwa Tanzania.

Amesema kuwa Maazimisho ya siku ya Mashujaa katika Makumbusho ya Taifa Mahenge ni muhimu sana kwa ajili ya kuwakumbuka  mashujaa wa Kingoni waliponyongwa kwa kamba hadi kufa na Wajurumani baada ya Watemi hao kukataa kufanyishwa kazi na Walowezi hao, ambapo sasa eneo hilo pamejengwa mnara. Wa kuwakumbuka.
Pamoja na mambo mengine maadhimisho hayo yalianza mwa maandamano kuanzia kwenye mnara waliponyogewa wazee wa kingoni,ambapo paliwekwa silaha walizotumia wazee hao zikiwemo,Nago.kishoka ( Kinjenje ),na Mkuki
Baada ya hapo kuelekea kwenye makumbusho ya Taifa ya Majimaji ambako kuna kaburi moja walilizikwa wazee hao wa kingoni wapatao 66,viongozi wa dini walitoa dua zao kuwakumbuka wazee hao.

No comments:

Post a Comment