Viongozi hao wa madhehebu mbalimbali walikuwa na mktano wa kujadili na kuweka mikakati ya kuwepo kwa amani nchini,baada ya na kable ya kikao hicho kulifuatia na maombi na duwa kutoka kwa viongozi hao.
Mwaenye kiti wa mkutano huo Shekhe wa Msikiti wa Jijini Dar es salaam kabla ya kufunga mkutano huo aliwasome wajumbe wa mkutano huo maazimio 10 yatokanayo na mkutano huo.Alisema viongozi wa dini tusiwe chanzo cha uvunjifu wa amani miongoni mwetu.Mitume wote walikuja duniani uleta amani kati binadamu.Aidha alisema mkutano huo ulikuwa wa viongozi wa dini wa Dar es salaam peke yao.
Mgeni rasmi mwenye kiti wa makampuni ya IPP Bwana Regnal Mengi alisema Tanzania ni kisiwa cha amani hivyo ni juu ya viongozi wa dini kuhubiri amani,ili taifa liwe na amani.'alisema nchi ikiwa haina amani wenye kutengeneza silaha wanafurahi kwa kuwa watapata soko la kuuzia silaha zao ili mmalizane'alisema Mengi.
Mashekhe,maaskofu,wachungaji wa jijini Dar es salaamu walichangia hoja hiyo.walisema serikali na viongozi wa dini wako mbalimbali,ndiyo maana kunapotokea jambo muumini akimuuliza kiongozi wake hajui,hivyo ni muhimu serikali iwe karibu na viongozi hao.
Baadhi ya viongozi wa dini wakisikliza kwa makini mazungumzo.
No comments:
Post a Comment