Thursday, February 24, 2011

WALIPONYONGWA NDUNA WA WANGONI NA WAKOLONI PAMEJENGWA MNARA WA MAKUMBUSHO



 ,Mnara huo kwa mbele ,hapa ni karibu na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma eneo la kihistoria ambapo viongozi wa kabila la kingoni waliponyongwa na wakoloni.
 Hapa nyuma ya mnara ambapo kuna nguzo na mwamba wenye kamba walizo tumia kunyonga viongozi wa kingoni.
 Mazingira ya mnara huo kama unavyo onekana kwa karibu.
Mzee Joseoh Henjewele mwenye fimbo ambaye pia alikuwa diwani mwanzilishi wa Mji wa Songea mwaka 1974,anasema tunaishukuru serikali kujenga kumbukumbu eneo ambalo babu zetu walinyongwa, lakini katoa anaglizo kuwa mnara ulivyo pakwa rangi ya kijani hakuleti uhasilia wa jambo lenyewe kihistoria ya wangoni.

Mahali damu ilimwagika ilitakiwa ipakwe rangi nyekudu ili kuondoa dhana ya mnara huo vinginevyo inaonyesha ni wa kumbukumbu ya kuzaliwa,kwa,CCM  kwani rangi zilizopakwa zimepoteza maana kabisa kwa tukio la kunjingwa kwa wangoni mahali hapo.

No comments:

Post a Comment