Sunday, February 6, 2011

MTOTO MLEAVYO NDIVYO AKUAVYO

 Padre Luxford Lugongo ambae ni mkurugenzi wa vijana jimbo la Songea aliwaasa wazazi kuwa na malezi mema mbele ya watoto wao,jinsi watakavyo tukanana,kugombana hata kupigana mbele ya watoto,na wao pia watafanya kama vile wazazi wao wanavyo fanya.hayo yalikuwa ni baadhi ya mahubili yake.katika jumapili ya  5 ya mwaka A.

Aidha alisema watu wawe chumvi baina yo katika maisha,alisema kila mmoja awe chumvi katika maisha yake,kwakuwa chumvi huifanya mboga iwe na ladha.Baba anatakiwa kuwa chumvi katika nyumba vivyo hivyo na mama anatakiwa awe chumvi katika familia.
Hii ni kwaya ya kigango cha Matarawe manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.iliyoimba katika ibada ya leo.

No comments:

Post a Comment