Saturday, February 5, 2011

MANISPAA YA SONGEA SASA MAMBO POA KIUSAFI

Manispaa ya mji wa Songea ilikuwa ikinuka kwa uchafu katika kila kona na Manispaa hiyo sasa ikombioni kuwa safi na kurudisha hadhi yake ya kuwa safi kama miaka ya Nyuma wakati Mstahiki Meya Ally Manya akiwa mwenye kiti wa Council hiyo. Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Mstahiki Aliy Manya alisema hayo leo kwenye ukumbi wa Maliasili mkoani Ruvuma wakati akifunga mdahalo wa wadau wa habari na waandishi wa habari kuhusu uhuru wa kutoa na kupata habari.kwa wandishi wa habari na wadau wa habazi zaidi ya 30 walio hudhuria mdahalo huo. Mheshimiwa Manya alisema tangu ameingia kwenye wadhifa huo mda mchache tu ameanza kushughulikia suala la usafi, ambapo maguba 26 yamesha malizika kutolewa uchafu kwa kutumia magari mawili ya manispaa na magari kukodi ya watu ili kumaliza kelele za wakazi wa manispaa hiyo juu ya uchafu uliyo tapakaa. Aidha amesema ameshatia saini mikataba ya ukandarasi wa ujenzi wa barabara na mikataba mingine ameikataa kusaini kwa kutoridhika na wakandarasi hao mpaka ahakikishiwe na wataalamu wa Tan Road .Baada ya usafi na barabara hatua itakayofuatia ni kuweka mazingira ya standi ya magari kuwa mazuri, Meya huyo ametoa wito kwa wadu wa habari kutoa habari kwa waandishi wa habari,na waandishi wa habari kabla ya kuandika habari na kuitoa kwanza waifanyie utafiti wa kutosha kutoka kwa mhusika kabla ya kuitoa habari yenyewe. Hatimaye kaomba ushirikiano uliopo kati ya waandishi wa habari na wadau wa habari uliyopo mkoani Ruvuma uendelee kudumu ili kuleta maendeleo ya Manispaa hiyo kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. ‘ ukitaka mambo yako yafanikiwe washirikishe waandishi wa habari,sio uwakimbie’ alisema Mstahiki Meya huyo.

1 comment:

  1. Tujifunze kutoka kwa wenzetu wa mji wa Moshi, ambao una sifa ya kutunza usafi. Nimeuongelea mji huo hapa.

    ReplyDelete