KILIMO KWANZA mkoani Ruvuma kauli hiyo itafanikiwa kwa kiasi kikubwa,msimu huu mavuno ya mahindi yanatarajiwa mavuno mengi.Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe. Dr.Christine Ishingoma amesema kuwa mwaka huu inategemewa kuvuna Tani 1,500.
Mavuno yatakuwa mengi kwa kutumia mbolea za kupandia za minjingu na mbolea za kukuzia ambazo zinafanya mahindi yanakuwa mausi na kupata mazao mengi.kwa sababu ya mbolea ya ruzuku ya serikali inayotolewa ingawa kuna kasoro ndogondogo zilizojitokeza za ubadhilifu wa vocha hizo.
Mkoa wetu umebarikiwa sana kwa hilo, na nawapongeza wana-Ruvuma kwa kukaza buti namna hiyo na kuipeperusha bendera ya Ruvuma katika uzalishaji wa chakula.
ReplyDeleteHongera zako Mzee Sikapundwa, kwa kazi kubwa unayofanya kuishughulikia blogu hii. Inavutia jinsi unavyoleta taarifa za mara kwa mara na kuwajulisha walimwengu yanayotokea mkoani mwetu na pande zingine za nchi.