Tuesday, February 1, 2011

BREAKING NEWS,UKATILI WA BINADAMU SASA UMEVUKA MIPAKA,HATA KWA AKILI YA KAWAIDA MAITI ZA WATOTO 10 KATIKA SHIMO MOJA NA SI KABURI UNAELEWA KITU KWELI HAPO?

 Tukio la kusikitisha lililotokea jana Mwananyamala kwa Kopa la kukuta watoto 10 wakiwemo 5 wakiume na 5 wakike katika shimo moja kwenye shuka ya hospitali ya Mananyamala.hivyo wewe kama binadamu uanaelewa kitu hapo?.

Hao ni mashuhuda waliofika katika tukio hilo,Huyo mzee anasema katika umri wake wote wa kuishi katika dunia hii hasa Tanzania hajawahi kukutana na unyama na ukatili kama huo,Hebu tujiuleze maswali je :-
  • Inawezekana watoto hao walizaliwa katika hospitali na kutupwa katika shimo hilo ,mama zao walikuwa wapi?
  • Ni kweli inawezekana kuna baadhi ya akina mama wanatupa watoto,je hao akina mama walikutana na kuwatupa watoto hao kwa pamoja?
  • Mkunga wa zamu siku hiyo inawezekana watu wasio na huruma walimwibia watoto hao wakati yeye yuko ofisini kwake,lakini mama za watoto hao pia walipewa dawa za usingizi wasijue kilichotokea?
  • Lakini cha kusikitisha hadi jana hiyo hakuna mama hata mmoja aliyekwenda kituo cha Polisi  cha Mwananyamala kuripoti kuibiwa mtoto wake,huoni hapa kuna siri kwa akinamama hao Dar.?
  • Nakama kweli watoto hao walizaliwa katika hospitali ya mwananyamala mganga mkuu ametoa taarifa ya kutoweka kwa watoto wachanga 10?
Amekweli binadamu hatuna huruma kuwaua watoto wasio na hatia,hawajala kitu cha mtu.Lakini mama huyo na baba wa watoto hao kama walikuwa hawana uwezo wa kutunza watoto hao kwanini walichukua uamuzi wa kuwaleta duniani na kuwaadhibu?.
Na huyo bwana ni mmoja wa wafanya kazi wa hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam,jina lake analijua mwenyewe,aanadai yeye si msemaji mkuu,msemaji ni mganga mkuu,polisi na vyombo vya usalama.Ni kweli yeye hausiki na tukio la kutisha kama hilo.Wewe na mimi tuangalie vyombo vya dola vitachukua hatua gani?. wataweza kuwabaini akina mama 10 walio wazaa watoto hao.

No comments:

Post a Comment