Thursday, February 17, 2011

KUSINI NA HISTORIA YA HIASHARA YA WATUMWA USULTANI TUNDURU KABILA YA KIYAO

 Masultani na Machifu bado wapo katika wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma ,hapo ni kundi la masultani wakiwa katika Taasisi ya KIUMA inayo endeshwa na Daktari Matomora.aliye amua kuanzisha Taasisi hiyo kwa lengo la kuondoa ujinga wilayani humo.
 Sultani Mpelembe ni Myao wa Malambo - baba yake wa kwanza aliitwa Chuma - Chekulungu ( maana yake ni chuma kikubwa).Kupitia masultani hawa hapo zamani biashara ya watumwa ilishamiri sana uyaoni,ikiwa ni pamoja na pembe za ndovu kwa kufanya misafara mirefu kati yao na Kilwa Karne ya 19.Livingstone alishuhudia wayao wakiteka watumwa nchini malawi katika mto Shire mwaka 1859.

Alipitia machifu kadhaa walioshughulika na biashara hiyo,na kujenga utawala wa kichifu karne ya 19 lakini haukudumu.Bishara hiyo ilidumu kwakuwa walikuwa na ushirika na watu wa pwani ,Kilwa na Afrika ya Kati.
 Kijiji cha Wayao na jinsi wanavyo karimu wageni wakiwatembelea nyumbani kwao,ngoma ,vyakula  vitaandaliwa,utamaduni wa kiyao ni wa Kibantu kwa ukarimu,Ila biashara ya kuuza binadamu na kufuata mila na desturi za kiarabu na ufuasi wa kiisalamu ndipo kulikorudisha nyuma maendeleo ya elimu Wilayani humo.

Watoto wilayani Tunduru,wameathirika kwa kiasi kikubwa katika elimu inayochangiwa na wazazi wao ambao wanaona elimu sio kitu cha kuwasaidia katika maisha,utoro,mimba,biashara ndogondogo ndizo zilizotawala miongoni mwa watoto hawa.

No comments:

Post a Comment