Friday, February 25, 2011

TAMASHA LA KUMBUKIZI YA MASHUAA WA VITA VYA MAJIMAJI NA UTALII WA UTAMADUNI LIMEANZA LEO MJINI SONGEE

 Tamasha hilo limeanza na wageni mbalimbali kutoka Tanzania na Msumbiji,wanaoingia ukumbi wa Songea Club Ni Mhe.Dr Christine Ishengoma Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katikati, mwenye kiti wa Bodi ta makumbusho ya taifa Dr.Constancia Rugumanu Kulia na katibu Mkuu wa Wizara mali asili na utalii  kushoto.

Kaimu RAS mkoa wa Ruvuma Dr.Tarimo akimkaribisha Mwenyekiti wa bodi ya makumbusho ya taifa Dr.Rugumanu,kutambulisha wageni,aliwatambulisha wageni wengi akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Ujumbe kutoka Msumbiji na wageni wengine.
 Mwenyekiti wa Bodi ya makumbusho ya Taifa Dr.Onstancia Rugumanu akitabulisha wageni katika ukumbi wa songea club leo.
 Katibu mkuu wizara ya maliasili na Utalii akisalimia wajumbe na wanakamati wa sherehe.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Lichinga Nchini Msumbiji Mhe.Augusto Assifue na ujumbe wake wa watu watatu waliyo wakilisha nchi ya msumbiji.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora bwana Abedi Mnyemusa akisalimia wajumbe wa maandalizi ya Tamasha.
 Mkuu wa wilaya ya Nkansi Mkua wa Rukwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo Bw.Daniel Ole Njolai
Chifu wa kingoni Bambo Emmanuel Zulu Gama akiwasalimia wageni na wajumbe wa Tamasha hilo,ambalo limeanza na ziazra ya kutembelea vivutio vya utalii vya :-
  • Chandamali.
  • Luhira
  • Peramiho
  • Maposeni,baada ya kukabidhi gari kituo cha Makumbusho ya majimaji cha Songea.kilele ni siku ya tarehe 27/2/2011.katika mnara walionyongwa machifu wa kingoni.Ambapo kutawekwa silaha za kijadi,mashada ya maua.na kuonyesha kazi za mikono.

2 comments:

  1. Asante kwa kutuletea yanayojiri. Napenda nisema, vivutio vya utatalii viwekwe wazi siyo kutaja tuu maeneo. Mfano ukisema Maposeni ni nini? Ni majengo ya mahakama, makazi ya Nkosi au himaya ya kale ya Nkosi kule ndirima. Tunapenda kujua vivutio vyetu!!!!

    ReplyDelete
  2. Ahsante kwa kutujuza kuwa ni wakati huu wa kusherehekea na pia kuitangaza Songea yetu.

    ReplyDelete