Wednesday, February 23, 2011

HOMSO/ HOSPITALI YA MKOA SONGEA KIPINDI KIFUPI CHA MGANGA MKUU DANIEL MALEKELA

 Daktari Daniel Malekela akitoka jengo jipya la wazazi ambalo lina chumba cha upasuaji wa mama mjamzito aliyeshidwa kujifungua mwenyewe.Daktari Malekela anasema kwa siku watoto 30 huzaliwa katika Hospitali ya mkoa  Songea.
 Kwa muda mfupi tu wa uongozi wa mganga mkuu huyu wa mkoa Daktari malekela kwa uongozi wake na staff yake na uongozi wa mkoa ameweza kubadilisha mazingira ya Taasisihiyo ya Afya ya mkoa wa Ruvuma kwa kufanya ukarabati mkubwa na kujenga majengo mengine mapya likiwemo hilo la ghorofa na jengo la wazazi. 

 
Majengo yaliyofanyiwa ukarabati mkubwa ni pamoja na jengo la upasuaji la zamani pamoja na OPD na majengo mengine ambayo Mganga mkuu huyo alimtembeza mpiga picha wa Blog hii kujionea maajabu.

No comments:

Post a Comment