Thursday, February 24, 2011

MWANAFUNZI WA MIAKA 12 KUWA MKE WA TATU WA MZEE VISENTI HAULE

Binti wa miaka 12 katikati Veronika Charlle wa darasa la tano, akiwa na mwenye kiti wa kijiji cha Sinai Talisis Mkanula na mhudumu wa afya  msingi Christina Njovu.walijaribu kumsaidia mtoto huyo lakini kukawa na urasimu wa kushindwa kumchukulia hatua mtuhumiwa Bwana Vinsenti Haule kwa kesi ya ubakaji maana huyu mtoto ni sawa na mjukuu wake.


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Vinsenti Haule mkazi wa kijiji cha Sinai Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma ambaye ana wake wawili amemuoa mwanafunzi  wa darasa la tano wa shule ya msingi Nakahuga  Veronika Challe(12) kuwa mke wake wa tatu.Imeripotiwa  na Albanos Midelo.

2 comments:

  1. Dunia hii sasa inakwisha jamani. Kweli mtoto wa miaka kumi na mbili, inasikitisha sana. Najiuliza kwa sauti hivi wanawake wamekwisha au ni nini? Ana wake wawili na bado anataka mmoja zaidi na ambaye analingana na mjukuu wake kweli huu uungwana. Hii si haki si haki si haki kabisaaa. Mwenga kyaniiiiiii????

    ReplyDelete
  2. Sheria ziko wazi, sasa urasimu unatoka wapi? kila mmoja wetu kwa nafasi yake awajibike tuliokoe taifa letu linalo zama katika dimbwi la mmomonyoko wa maadili.

    ReplyDelete