Friday, February 18, 2011

MAKAO MAKUU YA JESHI LA WANANCHI TANZANIA UPANGA KUONGEA NA WAANDISHI WA HABARI LEO

Mkuu wa wa usalama na utambuzi  Brigedia Jenerali Paul Meela ametota taarifa ya kwanaza kufuatia milipuko ya mabomu  Gongo la Mboto juzi,  kwawaandishi wa habari makao makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania Upanga  kuwa Ghala namba 5 ndiyo lilianza kulipuka,saa 2.30 usiku ndipo maghala yote 23 yalilipuka hadi saa 10.30 alfajiri na kuleta maafa  ya watu 20 na majeruhi 335.

 Alisema Taifa limepata hasara kwa wananchi walioyo poteza maisha yao na majeruhi waliyo athirika katika tukio hilo.Alisema ni mapeme mno kujua chanzo chake ila wananchi wawe na subira kupata chanzo cha milipuko hiyo.
Alisema mabomu yanaweza kulipuka kwa sababu mbalimbali kama hali ya hewa,uzembe au kulipuka yenyewe.
 Waandishi wa habari walitaka kujua kuwa matatizo kama hayo yanajirudiarudia ,kuna nini,kama ndivyo wanachukuliwa hatua gani waliokuwa wakilinda siku hiyo ?
 Brigadia Jenerali Leonard Mndeme,aliwaambia wandishi wa habari kuwa si kweli mabomu yalihifadhiwa kama mahindi,bali mabomu hayo yamehifadhiwa kitaalamu na wanayo yatunza ni wa taalamu wa milipuko.

Aidha alisema kuwa matukio kama hayo yametokea Zambia,Mozambiki,ni jambo la kawaida mabomu kulipuka,bila kutambua kuwa sasa yanalipuka.
Waandishi wakadadisi kuwa isiwe ni hujuma tu ilifanyika kati ya wapiganaji kwa kuto kuchukua taadhari ya milipuko hiyo,au siasa imeingia majeshini.

Idha Brigedia Jenerali Paulo Meela alisema watu 4,000,000 walifika uwanja wa uhuru kutamba ndugu  zao,majeruhi walipelekwa katika hosipitali za Temeke,Amana na Mhimbili. Amewataka wananchi kuacha kuokota kitu wasicho kifahamu.

No comments:

Post a Comment