Thursday, February 3, 2011

Idadi kubwa ya watu wazima , Vijana na watoto hawajui kusoma

 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Phillipo Mulugu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ripoti ya Kimataifa ya usimamizi wa Mradi wa Elimu kwa wote yenye  madhumuni ya kuwafikia waliotengwa.


Ripoti hii ilizinduliwa na UNESCO katika maadhimisho ya Elimu ya Watu Wazima.Aliyeshika kitabu kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima Bwana Saluum Mnjagila
 Mkurugenzi wa UNESCO nnchini Vibeke Jensen akizindua Ripoti ya Kimataifa ya Mradi wa Elimu kwa Wote inayojulikana kama ' kuwafikia waliyotengwa' katika sherehe za Juma la Elimu ya Watu Wazima zilizofanyika  wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani tarehe 18 Januari 2011.
 Njia shirikishi inayofundishwa na MUKEJA inawaletea walengwa yale waliyo tarajia,Hawa ni kikundi cha MUKEJA wakionyesha mazao yao waliyo yapata kutokana na shughuli wanazozifanya.Mkuranga.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe.Phillipo Mulugu akipata maelezo kutoka kwa mwanakikundi cha MUKEJA walivyofanikisha kutoka kilimo cha bustani alipotembelea katika banda lao la maonyesho. siku ya Juma la Elimu ya Watu Wazima Mkuranga Pwani.


IDADI kubwa ya watoto na vijana wenye umri kati ya 11 hadi 18 hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu  ama kwa kutoandkishwa au kuacha shule,kundi ambalo ni kubwa la wananchi wenye nguvu ambao wangeweza kuleta mchango mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kauli hiyo aliitoa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Pillipo Mulugu wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani kwenye kilele cha maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima mwezi Januari mwaka huu.

Mhe.Mulugu alisema ilipofikia mwaka 1986 idadi ya watu wasiojua kusoma ,kuandika na kuhesabu ilipungua hadi kufikia watu 1,366,721 sawa na asilimia 9.6, mbapo sasa asilimia hiyo imepanda siyo kwa watu wazima pekee,bali na watoto na vijana walioacha shule kwa sababu mbalimbali.

Kutokana idadi hiyo serikali imetoa fursa ya kuwapatia elimu wananchi ili kuboresha maisha yao,ndipo mwaka 2002 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilianzisha Mpango wa Uwiano Kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii ( MUKEJA ) ambao sasa umesambazwa nchi nzima ukitumia nja shirikishi katika kujifunza mambo waliyo yaibua katika kikundi chao.

Ndipo serikali ya Tanzania ikishirikiana na wataalamu kutoka nchini CUBA wameandaa Programu ya “ Ndiyo Ninaweza” Yes  I can itakayo fundishwa kupitia redio,televisheni na video,Programu hiyo ikikamilika itatoa ujuzi wa kusoma,kuandika na kuhesabu kwa wananchi watakao jiunga nayo.Programu hii pia itatoa maarifa na staid katika maisha ya kila siku.

No comments:

Post a Comment