Monday, May 2, 2011

Halmashauri na wazazi wametakiwa kukamilisha vitanda na ujenzi wa choo ndani ya ,mwezi

 Naibu Waziri wa Elimu TAMISEMI Mhe.Kasimu Majaliwa alisema kuwa alisikitishwa sana alipokuta matandiko ya wanafunzi yako chini kwatokuwa na vitanda vinavyo gharimu shilingi 3,000,000 katika hosteli ya wasichana.Na choo cha aina yake cha nyasi kama haitoshi hata usafi katika choo hicho hakuna.
Kutokana na hilo amemwambia Mkurugenzi Mtendaji,Afisa elimu sekondari kutengeneza vitanda vya double darker ndani ya mwiezi miwili viwe tayari.Wazazi wafue tofali  na kuanza ujenzi wa choo,Halmashauri itawapelekea bati
 Hicho ndicho choo cha hostel ya Lupunga sekondari watoto wa kike wanatumia,je ni kweli wanakijiji walikuwa hawaoni,kamati ya shule haikuona hilo mpaka Naibu Waziri afike?
 Hapo ndipo watoto hao wa kike wakilala chini vitanda hakuna,mwanafunzi huyo akishindwa mtihani wake utamlaumu,kumbe ni mengi yanamtatiza choo  ndicho ulicho kiona matandiko ndiyo hayo.Ufaulu utatoka wapi.
 Mheshimiwa Naibu Waziri hakuyaamini macho yake,kwenye ziara hiliyo atakutana na changamoto lukuki katika sekta ya elimu katika Mkoa wa Ruvuma.Huu ni mkoa wa 9 kufanya ziara za kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali.kwenye Sekta ya elimu.
Hilo ni bafu wanapo oga wanafunzi hao wanaoishi katika hostel hata usafi nao unahitaji fedha ukweli watu wanasema tembea uone,na wewe tembea katika Blog hii uone matatizo au changamoto zinazoikumba sekta ya elimu kuanzia elimu ya Msingi hadi sekondari.


No comments:

Post a Comment