Monday, May 2, 2011

MAAFISA ELIMU WILAYA WATAKIWA KUWEKA RATIBA YA KUZUNGUMZA NA WALIMU WAO

Naibu Waziri wa  Elimu TAMISEMI Mhe.Kasimu Majaliwa akipokea taarifa ya Elimu ya Mkoa wa Ruvuma katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ,leo kabla ya kuanza ziara yake
 Naibu Waziri wa Elimu TAMISEMI Mhe. Kasimu Majaliwa alizungumza na walimu,wazazi na wanzafunzi wa shule ya sekondari Lupunga Songea Vijijini baada ya kukagua majengo ya sekondari hiyo yakiwemo Hostel za wasichana na vyoo na kukuta mambo ya kusikitisha.
Mkuu wa Sekondari Lupunga Bibi Holiday Mwakasuka akisoma taarifa ya sekondari hiyo mbele ya Naibu waziri wa TAMISEMI alipofanya ziara yake siku ya kwanza leo katika wilaya ya Songea Vijijini Mkoa wa Ruvuma.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Lupunga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu TAMISEMI leo hii.






MAAFISAELIMU wa halmashauri za Manispaa na wilaya nchini wametakiwa kuweka ratiba ya kuongea na walimu wao kila mara,ili kuweza kupata matatizo ambayo yanawakabili walimu hao na kuweza kuyatafutia ufumbuzi.

Naibu Waziri wa Eimu TAMISEMI Mheshimiwa Kasimu Kajaliwa alisema hayo wakati akiongea na wakuu wa shule ,walimu wakuu na waratibu elimu kata katika ukumbi wa Songea Club leo baada ya kutembelea shule za sekondari za Lumunga  ya Songea Vijijini na Msamala ya maspaa ya Songea na luongea na wanafunzi.

Mhe.majaliwa amewaambia maafise elimu wakishirikiana na wakaguzi,TSD na taaluma katika wilaya kuongea na walimu wao kuepusha maswali ambayo yasingeulizwa kwa waziri kama wangeongea na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao.

Aidha Mhe.Majaliwa ameanza ziara ya wiki moja katika mkoa wa Ruvuma ili kukagua na kubaini maendeleo ya elimu pia kupata maoni na changamoto zinazorudisha nyuma jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu nchini.

Mhe.Naibu waziri ameanza ziara yake katika Halmashuri ya Manispaa ya Songea na Wilaya ya Songea Vijijini na kuongea na walimu,kesho ataelekeza Wilaya ya Tunduru ,kesho kutwa atafanya ziara Tunduru na kurudi Wilaya ya Namtumbo.kisha atakwenda Wilaya ya Mbinga na kufanya majumuisho tarehe 6 mwezi huu Songea Club.



No comments:

Post a Comment