Monday, May 23, 2011

BADRA ATAJA SABABU ZA KUKATIKA UMEME MARA KWA MARA

 Meneja wa  husiano wa TANESCO Badra Masoud amesema tatizo la kukati kwa umeme mara kwa mara ni kwa sababu ya uchakavu wa mitambo yake inayo tumia umeme wa maji.Alisema umeme wote unaozilishwa unatumika hakuna umeme wa ziada.Aidha alisema mgao unaoendelea sasa si wa TANESCO ni kwa sababu ya matengenezo ya mitambo ya umeme wa gesi Songosongo..Amesema umeme unaotumika hivi sasa ni MEGAWAT 350,na umeme wote wa maji,mafuta,na gesi unaozalishwa ni MEGAWAT 750
Amesema kuwa mitambo hiyo ni ya siku nyingi na kuifanyia ukarabati ni gharama kubwa ni bora kununua mitambo mipya .alisema umeme wote unaozalishwa ni kutoka kwenye vyanzo vya maji,mafuta na gesi.




1 comment:

  1. Nimeona kuwa wenzetu huku Marekani kiasi fulani cha umeme wanazalisha kwa kutumia upepo. Hata kwenye chuo nilipo kiasi fulani cha umeme huzalishwa kwa namna hiyo. Mtambo uitwao kwa ki-Ingereza "wind-turbine" unazungushwa na upepo na kuzalisha umeme.

    Tanzania, kama nchi zingine, tuna rasilimali hii ya upepo ambayo ni ya bure, kama vile ilivyo rasilimali ya jua. Kwa nini tangu tupate Uhuru hadi leo, akili yetu iko kwenye umeme wa maji, mafuta na gesi tu?

    Tungekuwa makini, angalau tungetambua kuwa upepo na jua ni nishati endelevu, tena hazina madhara katika mazingira kama haya mafuta na gesi.

    ReplyDelete