Monday, June 6, 2011

USAFIRI WA NDEGE TOKA DAR ES SALAAM KWENDA SONGEA UMEANZA LEO

 Ndege ndogo zinatua katika kiwanja hiki cha Ruhuwiko Songea Ruvuma
 Na ndege kubwa pia zinatua katika uwanja huu,Songea ina uwanja mzuri wa ndege,ila bahati mbaya ni ndege  za viongozi ndizo zinazo tua hapo,sasa imekuwa bahati kampuni hii imeamua kuanzisha huduma hiyo ya usafiri.
Maneja wa uwanja wa ndege Songea Bwana Valentine Fasha mwenye tai nyeusi akiwa na mfanyakazi mwenzake wakati Rais Kikwete akiwasili uwanjani hapo juzi.


KAMPUNI  ya ndege ya Air Indigo imeanza safari zake Leo,toka Dar es salaam kwenda Songea,ambapo toka juzi abiria kutoka Dar es salaam kwenda Songea walikwisha jaza ndege inayoweza kuchukua abiria 25.

Meneja wa uwanja wa ndege wa Songea Bwana Valentine Fasha  aliiambia blog hii uwanajani hapo kuwa nauli ya kwenda na kurudi ni Tanzania shilingi 400,000/=,pia alisema usafiri wa ndege utakuwa wa siku mbili Juma tatu na Ijumaa.

Alisema kuwa booking ya safari inafanyika hapo hapo Air port kwani kwa muda huu hawana na ofisi ya kukatia tiketi mjini Songea.Hizo ndizo habari njema kwa wakazi wa Songe,na wilaya zake.

1 comment:

  1. Ahsante kwa habari hii na kwa kueneza habari hii nimeiweka hapa kwangu pia Maisha na Mafanikio..Kunyumba.

    ReplyDelete