Thursday, June 2, 2011

'Mtoto wa mwenzako ni wako' Usemi huo umebainishwa kwa vitendo na mkuu wa shule Maposeni

Mkuu wa shule wa sekondari Maposeni Peramiho Mkoani Ruvuma Juzi amempokea mwanafunzi wa kidato cha kwanza aliyechaguliwa kusoma sekondari peke yake katika kata yao huko Magazini.

Mkuu huyo alisema kuwa mwanafunzi huyo karipoti hana sare,viatu,shuka hata ada,kwa madai kuwa wazazi wake walimchelewesha kufika shuleni kwa kukosa ada.Walikuwa wakusubiri kuuza mahindi mwezi wa 8 ndiyo akaende shule.

Kwa hiyo wakati wenzake wamefunga shule yeye anaripoti kwa  kuonewa huruma na mkuu huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja,alisema mwanafunzi huyo amebaki na wanafunzi wa vidato vya tano na sita akianakili yale wenzake wamejifunza.Ukweli mkuu huyo Mungu ambariki sana kwa kujitolea yeye na wenzake ili mwanafunzi huyo asome.


No comments:

Post a Comment