Viongozi
wa madhehebu ya dini mbalimbali nchini wameitaka serikali kuangalia upya
mikataba ya madini iliyo wekwa awali ambayo haimsaidii mwananchi kutokana na
mapato yatokanayo na madini hayo,badala yake huambulia kuona mashimo tu maeneo
yanapochimbwa madini hayo.
Tamko
la pamoja la viongozi hao wa madhehebu ya dini nchini lilitolewa na Jumuiya ya
Kikristo Tanzania (CCT ) ,Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania ( TEC ) na Baraza kuu la Waislamu
Tanzania ( BAKWATA ),wote kwa pamoja waliitaka serikali kutazama upya mikataba
ya madini kwa wawekezaji wa nje.
Aidha
Viongozi hao walitamka hayo hivi karibuni kuwa haki ya kikatiba haikuzingatiwa
kwenye mikataba hiyo ya madini, hivyo katiba haina budi kuandikwa upya ili
maslahi ya pande zote yazingatiwe.
Walisema
haki za binadamu katika maeneo ya migodi
haipo,haki za binadamu si suala la kisiasa,kama
kuna raia amefanya makosa hatua stahiki za kisheria zichukuliwe,sio vyombo vya
sheria vinaibuka na kuanza kuhatarisha
amani kwa raia wake.
Walisema
athari zilizopo katika sekta ya madini zisipotatuliwa mapema ni hatari kwa
umoja wa Taifa ( Source Mwananchi Juni 25 mwaka huu )
No comments:
Post a Comment