Sunday, June 5, 2011

SHEREHE ZA KUWEKWA WAKFU JOHN NDIMBO JIMBO LA MBINGA ILIKUWA HIVI

 Padre John Ndimbo alilala kifudifudi wakati Mwadhama Policarp Pengo akiendelea na sala
 Ni muda huo sala zilikuwa zikiendelea za kumwombea mteule huyo katika kanisa la jimbo la Mbinga leo
 Baada ya hapo ikafika zamu ya kuwekewa mikono na maaskofu wote
 Baada ya tende hilo alivishwa kofia ndogo nyekundu na pete
 Kisha akavishwa kofia kubwa kama unavyo shuhudia
 Baadaye akakabidhiwa fimbo
 Alivyo kabidhiwa fimbo ndipo Askofu John Ndimbo alipokuwa askofu kamili na akaenda kuto baraka yake ya kwanza kama askofu mpy wa Jimbo la Mbinga.
 Hata hivyo ulifikia wakati wa kumpongeza askofu huyo mpya wa Jimbo la Mbinga

Hatimaye Askofu  Paul Welnashery wa Ujerumani alisoma wasifu wa Askofu Ndimbo jinsi alivyo kuwa mwadilifu na kufikia daraja la uaskofu na kumkabidhi fimbo ya uchungaji.Mungu ambariki Askofu mteule John Ndimbo wa jimbo la Mbinga

1 comment:

  1. Asante sana, Mzee Sikapundwa, kwa taarifa hizi. Mbinga ndio kwetu, na napenda ujue kuwa nimeguswa sana na yote uliyoweka hapa. Kama wanavyosema humo mitaani, ubarikiwe sana.

    ReplyDelete