Monday, June 27, 2011

TAMISEMI NI CHOMBO KIKUBWA SANA NA CHA MUHIMU KATIKA MAENDELEO YA WANANCHI

 Mheshimiwa George Simba chawene Mbunge  ( CCM ) akielezea umuhimu wa TAMISEMI katika kipindi cha Jambo Mjini Dodoma leo Kupitia TBC ,kuwa chombo hicho ni cha muhimu sana katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta mbalimbali nchini.

 Mheshimiwa Chawene alisema kuwa Ili chombo hicho kiweze kuwa na mafanikio katika kutekeleza miradi yake ni vyema Waheshimiwa madiwani wangepewa meno katika kufuatilia fedha zinazopelekwa kwenye Halmashauri zetu
 Mheshimiwa Regia Mtema mbunge Viti Maalumu CHADEMA,asema kuwa TAMISEMI ina watendaji wengi mmno  kama ilivyo maafisa tarafa watendaji wa vijiji kama VEO na WEO na Madiwani,ni bora wote hao waondolewe na majukumu yote waachiwe waheshimiwa madiwani.
Aidha Mhe. Mtema anasema kuwa visingizio vya kuwa Waheshimiwa madiwani wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa sababu hawaja pelekwa semina ya kueleweshwa majukumu yao hiyo si kweli.
Alisema mara mtu anapokwenda kuomba achaguliwe kuwa Diwani ama Mbunge anatambua wajibu wakekatika kuomba nafasi hizo isiwe kizingizio cha kushindwa kutekeleza kwa sababu hawakupelekwa semina elekezi,yote hayo ni matumizi mabaya ya fedha za serikali.(Source TBC kipindi cha Jambo).

No comments:

Post a Comment