Monday, June 6, 2011

MKUTANO WA NNE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUANZA KESHO

Wananchi wanasema nini kuhusu imani yao na Bunge hilo la Tanzania,ambalo masikio na mawazo yao yote yako katika mkutano huo muhimu kwani ukienda kinyume na matazamio ya watanzania basi imekula kwao.

Kila watu wana mitazamo yao tofauti na bajeti ya mwaka huu:wengine wanajiuliza,je bajeti hii itakidhi mahitaji ya mwananchi wa hali ya chini kabisa?,wananchi wa maisha ya kati nao wanajiuliza je bajeti hiyo inaweza kupunguza mfumuko wa bei ya vitu muhimu katika maisha ya watanzania wa ngazi zote ?

Wengine wanajiuliza mkutano huu wa nne wa bunge la BAJETI lita kuwa Bunge lenye maadili mema kwa wapiga kura wao? au lugh ya funga mlango tupigane itaindelea? au tumechoka kuburuzwa itakuwa ndiyo mtindo wa Bunge hili?.Mbunge alivyo chaguliwa na wapiga kura wake walitegemea wametengeneza kisemio chao ndani ya Bunge kwa kuwa wote hawawezi kwenda ndani ya jengo hilo..

Kutokana na utaratibu huo ndiyo maana kuna uchaguzi wa Madiwani kwa visemea vya wananchi katika mabaraza ya Halmashuri ,vivyo hivyo na wabunge wetu.Sasa wanapo onyesha kwenda kinyume na matazamio ya wapiga kura wao ndani ya Bunge wananchi wanakuwa na mashaka nao.

Marumbano ndani ya Jengo lile ni kinyume na matazamio ya wananchi ,ila matazamio yao ni kuwa na lugha moja ya kumtoa mwananchi katika hali yake ya mashaka ya maisha,sio kuonyesha umwamba wa kusema na kubishana na Mhe.Spika ,kelele mtindo mmoja nidhamu imetoka Bungeni sio Siri,Amani na Utulivu unaoimbwa uanzie ndani ya Bunge letu,utofauti wa vyama sio kutengeneza mazingira ya kumnyima haki mpiga kura katika majimbo.

Kwa hiyo ili kupata bajeti itakayo jali hali ya maisha ya mwananchi,ni lazima kutetea hoja zao kwa mipaka ya kuheshimu Bunge lenyewe na kumuheshimu Spika wa Bunge ili afanye kazi yake kwa raha sio kwa karaha.

No comments:

Post a Comment