Wednesday, June 1, 2011

MWENDO KASI WA MABASI YATATUMALIZA AJALI NYINGIE YA ABOOD TENA LEO MLIMA NYOKA MBEYA

Mwendo kasi wa madereva wa mabasi yaendayo masafa marefu yatatumaliza kwa kusababisha ajali kwa mwendo kasi.habari hivi punde toka blog zetu Mzee wa matukio zinasema ajali nyijgine imetokea eneo la mlima nyoka Mkoani mbeya iliyosababishwa na basi la kampuni ya Abood  la kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya na abiria 36 wamepata majeraha na kukimbizwa Hospital ya Rufaa Mkoani humo.

Hata mwezi haujapita basi la kampuni ya Sumry lilisababisha ajali na kuua wasafiri 13 palepale,kabla famili na wanachi hawajasahau matukio ya ajali za mabasi leo tena.Madereva hawa watatumaliza jamani.Kwa nini dereva anakula mirungi wakati akiendesha gari?,kwa nini alewe? asikilize simu huku akiendesha basi? Na sie abiria kwa nini tunashabikia dereva akienda mwendo kasi?,ajali ikitokea huyo huyo anamlaumu dereva ,nani mwenye kosa? alisikiliza ushabiki na akafanya kweli kwa nini ulie?

No comments:

Post a Comment