Wednesday, June 1, 2011

KIJIJI CHA MATUMAINI MKOANI DODOMA NA IKONDA WILAYA YA MAKETE MKOA WA IRINGA NI UKOMBOZI WA WATOTO WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI

Vituo vya mashirika ya kidini ya Roman Catholic vya kijiji cha matumaini katika manispaa ya Dodoma kinalea watoto wenye kuishi na virusi vya UKIMWI,kuwapa lishe,tiba na elimu kuanzia chekechea hadi sekondari,pamoja na kituo cha Ikonda kilichopo  Wilaya ya Mkete mkoa wa Iringa nacho kina tunza watoto wenye matatizo hayo.
Watoto wanao lelewa katika vitu hivyo ni miongoni mwa 1,600,000 wanaishi na virusi vya UKIMWI nchini,kwa mujibu wa taarifa ya Tack Aid.Waziri wa Afya Dkt Haji Mponda anasema hadi sasa hakuna dawa ya UKIMWI.
Kuhusu tiba ya babu huko Loliondo Dkt Mponda anasema hawezi kuthibitisha kuwa inasaidia kwa kuwa haija thibitishwa na shirika la afya duniani.
 

No comments:

Post a Comment