Thursday, June 9, 2011

JUBILEI YA DKT NORBERT MTEGA ASKOFU WA JIMBO KUU LA SONGEA ILIKUWA HIVIIIII

Muadhama  Kadinali Polikapi Pengo akitoa maelezo mafupi kuhusu Mungu alivyo Mjalia baraka Askofu Norbert Mtega kufikia miaka 25 ya uaskofu,38 ya upadre na 66 ya umri wake.
Masista wakimsikiliza Muadhama Pengo
Baadhi ya Maaskofu walioshiriki katika Jubilei hiyo ambayo imejumuisha maaskofu wote wa Tanzania Bara na Visiwani.
Maaskofu wenye umri mkubwa.

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es salam Muadhama  Kadinali Polikapi Pengo alisema kuwa Maaskofu na waumini walifika katika Ibada ile ya Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu,38 ya Upadre na 66 ya umri wa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Dkt Norbert Mtega.ili kumwombe kwa Mungu aweze kumuongezea maisha marefu katika kazi yake ya kitume.

Alisema mambo ni mengi lakini asitisike wala asikate tama,wala asikaze uso wake kama gumegume na akakata tama,ila azidi kumuomba Mungu ili amzidishie maisha marefu nao watazidi kumuombea Mungu ili afanye Jubilei ya miaka 50 ya Uaskofu.’Ila kwa kipindi hicho nitakuwa sina akili za kutosha’ Alisema Kadinali Pengo.

No comments:

Post a Comment