Tuesday, June 7, 2011

NGONO YA RUSHWA KWA MWANAFUNZI IMEMPELEKA GEREZANI MTU WA MUNGU WA KKKT IRINGA, IMEMSAIDIA RAIS KIKWETE KUJIBIA KWA MAASKOFU

 Picha ya Pamoja ya Mwadhama Kadinali Policalp Pengo,Rais Kikwete na Askofu mteule John Chrisostomu Kigenzu Ndimbo wa Jimbo la Mbinga mara baada ya hotuba ya Kikwete tarehe 5 Juni mwaka huu Mjini Mbinga.
 Rais Kikwete wakishikana mkono na Askofu John Ndimbo mara baada ya kuwekwe Wakfu kuwa Askofu wa Jimbo hilo Juma pili iliyo pita katika kanisa la Jimbo la mbinga.
Rais Jakaya Kikwete katika picha ya Pamoja na Askofu Mstaafu Emanueli Mapunda katikati na Rais Mstaafu William Benjamini Mkapa ikiwa ni kumbukumbu kwao wote.

Aidha Jumuiya ya kikristo imemtaka Rais kikwete awataje watu wa Mungu waliyo kamatwa na madawa ya kulevya kama alivyo sema wakati wa hotuba yake na maaskofu,mapadre,masista,watawa na viongovi wa Serikali,Mungu amemsaidia Rais kumjibia.

Rais kama Kiongozi wa nchi hawezi kusita kukemea maovu yanayofanyika na Binadamu,maana binadamu si mkamilifu,ni lazima aonye alisema kwa nia njema kuwa kuna baadhi ya watu wa mungu wamevutiwa na biashara hiyo, ' na tumewakamata' alisema.

Kiongozi mzuri ni yule anayeona maovu anakemea kuliko kusifia tu,Mbona alianza na kuwamwagia sifa watu wa Mungu , ' watu wa mungu hawajihusishi na mauaji ya walemevu wa ngozi na wenye macho mekundu' baadaye akamalizia na kuhusika na bishara ya madawa na ubingwa wa kuunda Passport  fake.Alipowa mwagia sifa wao hawa kumshuru,ila aliposema wana vutiwa na biashara haramu imekuwa ataje ndani ya masaa  48.

likina kabla hajajibu,Mungu kamjibia kupitia kwa Mtu wa Mungu huko Iringa aliyepelekwa gerezani kula ugali na watu ambao si wa mungu miezi sita kwa tuhuma za RUSHWA YA NGONO na MWANAFUNZI,mbaya zaidi  taifa limemkabidhi  watoto kuwalea badala yake anakuwa FATAKI kumbe MAFATAKI hawa hata watu wa Mungu wapo.Sasa kunatofauti gani ya bishara ya madawa ya kulevya na bishara ya ngono TENA NI RUSHWA ilimwanafunzi afaulu ,hivyo huyo ni mtungaji wa mitihani baraza la Mtihani la Taifa?.

Ni juu ya viongozi wa juu wa watu wa Mungu kwa madhehebu yote kujichunguza,pia kuwatathimini viongozi wenye madara waliyo wapa,na kisha wamwendee kwa upole Rais atawatajia sio kwenye vyombo vya habari,Akitaja ni aibu ya muhusika na aibu mbele za Mungu kujifanya mtu wa Mungu kumbe anatengeneza kivuli cha kufichia maovu mbele ya jamii na wafuasi wake.Rais endelee kukemea maovu sio kwa watu wa Mungu peke yao bali hata kwa  wale aliyewapa dhamana ya kumsaidia.



No comments:

Post a Comment