Friday, June 3, 2011

BURUDANI YA LIZOMBE HAIKUWA NYUMA KATIKA MAPOKEZI YA MAKAMU WA RAIS UWANJANI HAPO

 Hicho ni kikundi cha lizombe cha Lizaboni Songea ,wakitumbuiza wakati walipompokea makamu wa rais uwanjani hapo Ruhuwiko hivi karibuni mjini Songea.

 Kama hujakuta lizombe ujuwe hujafaidi Songea,hii ni ngoma maarufu sana mkoani hapa kwa shughuli mbalimbali za kitaifa na za kimila kwa kusherehesha, Dkt Bilali akimsikiliza mmoja wawaimbaji katika kikundi hicho cha lizombe wimbo wenye ujumbe wa kutunza mazingira.

 Hawa ni wazee wa Kingoni na Ngoma yao ya Ligiu,Ngoma hii inaasili ya Kizulu wanacheza huku wameshika ngao na kinjenje au kishoka cha kijadi.Na nyimbo zenyewe zenye Ghani ya kizulu.
Akina mama hawa walikuwa akimwimbua Makamu wa rais kumkaribisha Songea ,haya ndiyo mambo ya songea wiki iliyo pita.

2 comments:

  1. Shukrani kwa taarifa na picha hizi nzuri sana. Sikujua kama uwanja wa ndege wa Songea bado unafanya kazi, maana sijausikia kwa muda mrefu. Sijui kama safari za ndege bado zipo. Naamini tunazihitaji, kama wenzetu wa sehemu zingine za nchi.

    ReplyDelete
  2. Samahani imekuwa 'posted' kabla sijamalizia,ni kwamba kesho Rais Jakaya Kikwete atatua na viongozi waandamizi serikalini,kwa ajili ya kilele cha siku ya Mazingira Duniani kitaifa zinafanyika Songea,Pia kesho kuna kuwekwa wakfu Askofu wa Jimbo la Mbinga Rais amealikwa huko kwenye sherehe hizo.

    Kuhusu ndege kutua za abiria wa kawaida,Meneja wa ndege wa uwanja huo alisema kuwa Air Indigo wameonyesha nia ya kuanza safari zake kutoka Dar-Iringa na Iringa Songea.Mungu akipenda na sie tutafaidika.

    ReplyDelete