Monday, June 6, 2011

MGENI NJOO MWENYEJI APONE,NI UGENI WA MJI WA MBINGA HUO,WENYE NYUMBA WAMEFAIDIKA

 Usemi usemao kuwa mgeni njoo mwenyeji apone,umejidhihirisha katika mji wa Mbinga wiki iliyopita,kufuatia Sherehe ya kuwekwa wakfu Askofu Mteule John Ndomba wa Jimbo la Mbinga. Kufuatia sherehe hiyo nyumba zote za kulala wageni zilijaa hata zile za dezo zilijaa,ama kweli kukiwa na sherehe biashara inalipa.
Nyumba hizo zilijaa wageni kutoka ndani ya wilaya na nje ya wilaya,kwa hiyo wenye biashara za nyumba za wageni wilayani humo wamefaidika na sherehe hizo.Hao unaowaona ni baadhi ya waumini waliohudhuria ibada ya kuwekwa wakfu Askofu John Ndimbo jana kutokana na kanisa hilo kukosa nafasi ya kuingiza waumini wote kanisani humo.

No comments:

Post a Comment