Saturday, June 25, 2011

UKISHANGAA YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI

Ni kitu cha kawaida katikamaisha ya kilasiku kwa binadamu,Watu wanasema mkimbie binadamu kuliko simba anaweza akakusamehe.
Bali binadamu akikukamia jambo kuwa lisifanikiwe,atajitahidi hadi usifanikiwe,iwe kwa nguvu zake,fedha,Supernaturals power basi  ili  ikikosa kufanikiwa yeye anafurahi kuwa amamkomoa.Lakini ukifuatilia watu kama hao hawana ujira wowote katika kujituka kwao katika kuharibu.
Sasa  watu kama hao katika Jamii wanakuwa na nafasi gani?,je wanakuwa na usalama gani katika maisha yao ?,Watu wametofautiana katika busara,je wakiwafanyia mambo kama hayo kwa watu wenye busara hafifu watakuwa katika hali gani?Na wanapo waharibia wenzao  wao wananufaika na kitu gani?

Hayo ni matukio yanayowatokea watu wengi wanao paga mipangilio yao kisha ikaharibiwa na watu kama hao dakika za mwisho na watu wakabaikia midomo wazi.Je huo ni ungwana?

No comments:

Post a Comment