Thursday, June 9, 2011

NI DHANA POTOFU VIONGOZI WA SERIKALI KUSEMA WATAWAPELEKEA WANCHI MAENDELEO

 Rais Mstaafu William Benjamini Mkapa akihutubia Maaskofu,mapadre,watawa,viongozi wa serikali na waumini kwenye Ibada ya Jubilei ya Askofu Norbert Mtega katika kanisa la kiaskofu Mjini Songea leo.Maendeleo ya mtu huletwa na mtu mwenyewe.
 Baadhi ya Maafisa kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma
 Rais Mstaafu Mkapa na mkewe mkuu wa mkoa wa Ruvuma na wakuu wa wilaya na mwenye kiti wa CCM Mkoa
 Baadhi ya Maaskofu wakimpongeza mwana - Jubilei
Manaibu maaskofu waliowakilisha maaskofu na maaskofu










  • Viongozi wa serikali kuwaletea  wananchi maendeleo ni dhana potofu.

RAIS Mstaafu Benjamini Mkapa ammwagia sifa tele Askofu Mkuu wa waJimbo Kuu la Songea Dkt Norbert Mtega wakati akihutubia Maaskofu,Manaibu Maaskofu,Maabate,Mapadre,Watawa,Viongozi wa Serikali na waumini waliofika kwenye ibada ya Jubilei ya miaka 25,ya Uaskofu,miaka 38 ya upadre na 66 ya umri wake katika kanisa la Mathias Mulumba Kalemba leo mjini Songea.

Mkapa alisema kuwa Mtega ni mwanaharakati wa elimu sehemu zote alizofanyia kazi za kichungaji,kutokana na juhudi zake ameanzisha chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya Computer katika Manispaa ya Songea,na yuko mbioni kuanzisha chuo kikuu cha Kilimo mjini hapa  kupitia wafadhili aliyo wapata kwa jitihada zake.

Alisema Askofu Mtega ni mahili sana katika kuhubiri,kutokana na umahili wake katika kuhubiri,hawachoshi wasikilizaji wake. Alisema nachukua nafasi hiyo kuwashukuru mashirika yote yaliyomwezesha Askofu Mtega kuendeleza elimu.katika Jimbo lake Mungu awabariki kwa moyo huo.

Aidha alisema kitendo cha baadhi ya viongozi wa serikali  kusema kuwa watawaletea  wananchi maendeleo ni dhana potofu,’maendeleo ya mtu huletwa na mtu mwenyewe’ alisema.Serikali haiwezi kumletea kila mmoja maendeleo pale alipo bila ya kujituma kutafuata maendeleo.

Alisema watu waje kujifunza Jimbo la Songea na Mbinga waone watu walio omba kuendelezwa na sasa wajiendeleza wenyewe.Bila ya kuwategemea walioleta mendeleo kwao.

Pia alisema tuzidi kusali ili Sudani ya kusini na wao wawe huru,kwani mauaji,na maovu ya kinyama yanazidi kuendelea Sudani ya kusini amani hakuna,alisema kila mmoja wetu asali huwenda sala zetu Mungu akazisikia na amani ikapatikana nchini humo siku moja.
           
Rais Mstaafu Mkapa alikuwa katika shughuli za kuwekwa Wakfu Askofu John Ndimbo wa Jimbo la Mbinga.Jubilei ya Miaka 50 ya Uaskofu Mikaranga Abasia ya Hanga na leo Jubilei ya miaka 25 ya Uaskofu,38 ya Upadre na 66 ya umri wake Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Dkt Noebert W.Mtega. Mjini Songea.

No comments:

Post a Comment