Sunday, June 5, 2011

DKT.kIKWETE AYAFAGILIA MADHEHEBU YA DINI BAADA YA KUMWEKA WAKFU ASKOFU JOHN NDIMBO MBINGA

 Rais Dkt Jakaya Kikwete akiwahutubia Maaskofu wakuu,Maaskofu,Mapadre,Wasista,Watawa,Viongozi wa serikali na waumini wngine.katika kanisa ka Jimbo la Mbinga baada ya kuwekwa wakfu askofu John Ndimbu.
 Picha ya Askofu John Ndomba na Rais Dkta Jakaya Kikwete mbele ya kanisa la Jimbo la Mbinga leo.
 Picha ya Pamoja na Mwadhama Policalp Pengo wa kwanza kulia,na wa kati ni Rais Jakaya kiwete na wa mwisho mwenye fimbo ni Askofu John Ndimbo
 picha ya pamoja ya Mwadhama Policarp Pengo na Askofu John Ndimbo wa jimbo la Mbinga mbele ya kanisa la Mbinga
 Picha ya pamoja na Maaskofu wote,Rais Kikwete,Rais Mstaafu William Benjamini Mkapa,pamoka na mkuu wa mkoa  wa Ruvuma Dht Christine Ishengoma

Picha ya Pamoja ya Rais mstaafu Willium Mkapa Maaskofu Mwadhama Kadinari Policap Pengo na Askofu mteule John Ndimbo.


RAIS wa Jamhuri ya Tanzania Dkt.Jakaya kikwete ameyafagila madhehebu ya Dini kuwa ni  wenye kutenda mambo ya haki kila wakati,hivyo ni wajibu wa madhehebu hayo kukemea maovu katika jamii ili kuiweka nchi katika hali ya amani na utulivu.

Dkt Kikwete alisema hayo alipokuwa akihutubia Maaskofu,Mapadre,Masista,Watawa  na waumini baada ya kuwekwa Wakfu Askofu Mteule wa Jimbo la Mbinga Padre John Ndimbo na Mwadhama Kadnari Polcarp  Pengo katika kanisa la jimbo la Mbinga leo.

Rais alisema Serikali inayaamini madhebu yote ya dini bila ubaguzi kwa kuwa ni wacha Mungu.Alisema wacha Mungu si watu wezi,wabaguzi wa wenzao,ni watiifu wa sheria wala hawaonei wengine,wanathamini uhai wa wenzao kwa kutojihusisha na mauaji wa walemevu wa ngozi kwa tama ya utajiri.

Aliongeza kuwa wacha Mungu hawajihusishi na mauaji ya watu wenye macho mekundu kwa madaui kuwa watu hao ni wachawi,kwa hiyo wametakiwa kuhubili amani na utulivu na uadilifu katika jamii.

Aidha alisema wacha Mungu hawatumii muda wao kunywa pombe,au kushinda vijiweni kucheza  pool na kusubili maisha bora yawajie kama mvua bila ya kufanya kazi.alisema madhehebu ya dini yanaisaidia sana serikali,na serikali nayo iko tayari kuyasaidia madhehebu hayo bila kubagua.

Alisema kuwa katika mipango yao waweke kipaumbele katika ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi,kwani vijana wengi wanamaliza shule,kazi hakuna,lakini wajifunza stadi mbalimbali katika vyuo hivyo wataweza kujiajiri wenyewe.

Amemsifia Askofu Mstaafu Mapunda kwa kuinua elimu Wilayani Mbinga kwa ujenzi washule za Awali,Msingi, sekondari na chuo cha ufundi ambapo soko la ajira kwa vijana waliopitia ufundi stadi lipo wazi.

Kuhusu serikali Dkt Kikwete alisema kuwa imesha azimiakujenga chuo cha VETA katika kila wilaya  nchini,ambapo hadi sasa kuna Wilaya 21 zina vyuo vyaVETA na vyuo vya maendeleo ya wananchi 21.

Hata hivyo Dkt Kikwete amesikitishwa na baadhi ya watumishi wa Mungu ambao wanashawishika kuingia kwenye biashara ya madawa ya kulevya,na wengine           

No comments:

Post a Comment