Monday, June 27, 2011

BREAKING NEWS ABIRIA ZAIDI YA 600 WALIOKWAMA KWA SIKU TATU MKOANI TABORA KUANZA SAFARI LEO KUELEKEA KIGOMA KWA GARI MOSHI

Abiria waliokuwa wakisafiri kwa gari lamoshi  (Train ) Reli ya kati katiya Usinge na Nguruka kufuatia ajali ya gari la mizigo lililo anguka na kuziba njia, na kufanya gari la moshi kutoka Dar es salaam kwenda Kigoma na kutoka Kigoma kwenda Dar es salaam kukwama kwa siku tatu.
Wasafiri hao wanasema kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu kwa kuwa abiria walikabiliwa na matatizo ya :-
  • Huduma ya choo hakuna
  • kushindwa kuoga
  • Hakuna chakula
  • Hakuna maji ya kunywa
  • vitu vimepanda bei vikiwemo chakula na maji ya kunywa.
Abiria wanaokwenda Kigoma wameondoka leo saa 1.30a wale wanaoelekea Dar es salaam watasafiri siku ya Juma tano saa 2.30 asubuhi.( Source TBC ) Nico Mwaibale.

No comments:

Post a Comment