Leo ni siku ya Mtoto wa Afrika lakini kuna baadhi ya watoto,wako kwenye mazingira magumu,hatarishi,wanatumikishwa kazi kwenye migodi,kwenye uvuvi,kwenye ajira mbaya ya kuudhalilisha utu wao,wengine wamejiingiza kwanye madawa ya kulevya.
Lakini jamii inasema nini kuhusu watoto hawa,Pole kwa wale amboa wamepoteza wazazi wao wote,je jamii inawachukuliaje hawa?,lakini pia kuna baadhi ya watoto hawa wazazi wapo,wana nguvu,kutunza hawataki,waliwazaa wanini?
Watoto wanahitaji huruma yako na yangu,mtoto wa mwenzako ni wako,ingawa siku hizi usemi huo hauingii masikioni mwa watu,ukitamani kumweonya mtoto wa mtu anapokosea,utakijua kilicho mfanya mbwa abweke.Maana atakujia mama yake,shangazi shoga watakuanadama hata ukose amani.Lakini tusikate tamaa.
No comments:
Post a Comment